0
Sasa imethibitika rasmi kuwa Kris Jenner na mumewe Bruce Jenner wametalikiana baada ya kukaa kwa muda mrefu wakiwa wametengana.
Jaji wa mahakama ya mjini Los Angeles alisaini nyaraka hizo lakini hakua tayari kuziweka wazi mpaka itakapofika mwezi Machi mwakani ili kutimiza masharti ya takala hiyo kisheria ambayo ni mpaka baada ya miezi sita.
Kwa masharti ya talaka hiyo iliyoonyesha kuwa Kris ataendelea kuihudumia familia yake huku wakigawana mali za benki na mali nyingine na kisheria Kris anatakiwa kumlipa mumewe dola za Kimarekani milioni 2.5 ili waweze kulingana.

Wawili hao waliachana tangu Oktoba mwaka jana baada ya kudumu kwa miaka 22 ya ndoa yao.
“Tumeishi kwa kutengana lakini kila mmoja alikua na furaha na mwenzake na pia tulikua tunaheshimiana ingawa hatukua pamoja,siku zote tutaendelea kubaki marafiki na familia yetu tutaendelea kuipa nafasi ya kwanza,”Alisema Kris.

Post a Comment

AddThis

 
Top