WERRASON NGIAMA MAKANDA SIAMINI UCHAWI
Kwenye Mahojiano yake na Gazeti » La Prospérité » JIJINI KINSHASA, WERRASON NGIAMA MAKANDA LE ROI DE LA FORET, kasema : Mambo ya Uchawi na Mengine ya kishirikina hayana kabisa nafasi kwenye Muziki. Wala msidanganywe na yeyote yule, Takriban Miaka 30 niko kwenye Fani ya Muziki na haijawahi kutokea hata Siku mmoja nikaenda Kumuona Mganga wa Jadi au Mpiga Ramuli.
WERRASON kasema Wapo wale ambao walio wahi kutumia Uchawi ili wapate kungaa kwenye Muziki, Siwezi kuwataja kwa majina, ila Wengi wao Wamesha fariki. Na Wale ambao bado hawajazingatia somo hilo, sidhani kama Watafaulu kabisa kwenye Muziki.
Kaendelea kufunguka WERRASON kwakusema : Hakuna siri nyingine ya Mafaanikio zaidi na uchapaji vilivyo wa Kazi, Wala sio Uchawi utakao kusaidia kwenye Utunzi wa Nyimbo au Kwenye Utayarishaji na Utengenezaji wa Album.
Kwenu nyinyi VIJANA, acheni Papara, Tulieni na Sikilizeni Ushauri wa Wazee wenu, Fanyeni Kazi kwa Bidii na Matunda yake Mtayaona. Kazi ndo Msingi wa maisha.
WERRASON Anajihimiza na kawahimiza Wenzie wanamuziki kumrudilia Mwenyezi MUNGU, ndie Mpaji wa Riziki na Mtoaji wa Vipaji, Mafaanikio yake yatokana kwa Kiasi kikubwa na Sala na Maombi, Kamshukuru MKEWE » MAMA SYLVIE MAMPATA » kwa mchango wake Mkubwa kwenye maombi. ( MKEWE NI MCHUNGAJI WA KANISA ).
Mwishowe, WERRASON katoa challenge, Kwa Mtu yeyote alie na ushahidi Tosha kwamba kesha Muona yeye WERRASON kenda kumuona Mganga wa Jadi au Mpiga Ramuli, Basi asisite kupita kwenye Vyombo Vya Habari na Alikemee Jambo hilo Hadharani.
SIAMINI MAMBO YA USHIRIKINA, NIMEZALIWA KWENYE FAMILIA YA KIKRISTO, KWETU SISI MUZIKI UPO KWENYE DAMU, KWENYE UKOO, BABA YETU MZAZI ALIKUA PIA MUIMBAJI MZURI KIJIJINI KWAO. NDO MAANA MIMI NA KAKA YANGU » FRERE PATRICE » TUPO KWENYE ORODHA YA WAIMBAJI WANAO JULIKANA SANA INCHINI KWETU. INGAWA YEYE NI MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI.
WERRASON kasema, ALBUM » FLÈCHE INGETA » BILA SHAKA ITATOLEWA MWISHONI MWA MWAKA HUU 2014 , KAZI ILIOKUBWA TAYARI IMESHAMALIZIKA, KADHALIKA BAADHI YA VIDEO CLIP. NAWAOMBA MASHABIKI NA WAPENZI WA MUZIKI WAENDELEE KUVUTA SUBIRA.
Post a Comment