0
Wachezaji watatu wa Simba ambao walisimamisha na kamati ya utendaji wa utovu wa nidhamu na kucheza chini ya kiwango, jana hawakutokea kwenye kikao kilichotakiwa kuwakutanisha na viongozi wao.

Kikao hicho kilikuwa maalum kwa ajili ya viongozi kuwasikiliza na kutaka kujua nini kilitokea, kama wana makosa au la!
Baada ya hapo, uongozi ungekuwa na nafasi ya kutafakari na kuona makosa yalipo, halafu wahusika wangeadhibiwa au vinginevyo.
 CHANONGO

Wachezaji Amri Kiemba, Shabani Kisiga na Haruna Chanongo, wote hawakutokea katika kikao hicho.
Kisiga pekee, ndiye alipiga simu kutoa udhuru tena baada ya muda waliotakiwa kufika kwenye kikao kuwa umepita.
Awali niliandika makala, nikiwashauri viongozi wa Simba kutenda haki kwenye kikao hicho na kuwa makini wakiachana na hisia, badala yake waangalie usahihi kabla ya kufikia kuhukumu.
Lakini leo, nasema wazi nimeshangazwa sana na uamuzi huo wa akina Kisiga, Kiemba na Chanongo kuacha viongozi wao akiwemo Rais wa Simba, Evans Aveva anakwenda sehemu, anawasuburi, hawatokei halafu wanakaa kimya.
Ni picha mbaya sana, hali inayoweza kujenga hata hisia zisizo sahihi. Pili inaonyesha kweli wao ni watovu wa nidhamu.

 KIEMBA

Hakuna ambacho wanaweza kujitetea zaidi ya kuomba radhi. Huenda mwanzo hakukuwa na tatizo kwao na ingejulikana baada ya kukutana na uongozi wao.
Lakini sasa kuna tatizo, tena liko wazi kwamba wameonyesha utovu wa nidhamu. Hata Kisiga anaweza kuwa na nafuu, lakini alikosea.
Kiemba aliwahi kusema kama riziki imeisha Simba, basi! Sahihi, riziki hutoa Mwenyezi Mungu, lakini hata mara moja hajawahi kutoa utovu wa nidhamu.
Hivyo Kiemba alipaswa kwenda kwenye mkutano, alitakiwa kuzungumza bila ya woga na mwisho aache uamuzi utaotolewa. Kama angeonewa, basi kweli riziki ndiyo imeisha na Mungu angempatia nyingine.
Lakini kitendo cha kumuweka kiongozi mkubwa wa klabu ambaye amejitokeza kwenda kukusikiliza, sasa kunakuwa hakuna tena lawama kwake badala yake ni wachezaji.
Lengo la SALEHJEMBE si kutetea upande wowote, haki itendeke ndiyo muhimu zaidi.
Lakini msisitizo, kwa walichofanya Kiemba, Kisiga na Chanongo ambaye ni chipukizi, si kitendo sahihi na wanapaswa kujitathmini upya kwa kuwa katika dunia hii, hakuna aliyewahi kufanikiwa kwa ubora wa kiburi chake.

Post a Comment

AddThis

Top