0

Na Saleh Ally
MANCHESTER United wamejibandika jina la Mashetani Wekundu, wakitaka kuonyesha kuwa wao ni watu hatari, ukikutana nao uwanjani, ujue umekwisha.

Kwa zaidi ya misimu 15, Manchester United haijawahi kuwa na hofu ya juu dhidi ya wapinzani wao Manchester City kama ilivyokuwa msimu uliopita na huu wa 2014-15.
Man United, wana hofu, kila wanapokutana na jirani zao hao wanajua ni shughuli pevu na msimu uliopita walianza kuipata ‘fleva’ ya woga. Msimu huu imepanda juu zaidi kwa kuwa hawakiamini kikosi chao.
Kesho ni mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa msimu huu ambayo inawakutanisha wapinzani hao wakubwa wa Jiji la Manchester, huku Man City wakiwa nyumbani kwao Etihad.
Tayari wameharibu mara mbili mfululizo, wamefungwa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham, wakavuliwa ubingwa wa Capital One Cup kwa kufungwa na vibonde Newcastle. Sasa wakubali tena kuendelea kuwaudhi zaidi mashabiki wao kwa kupoteza “Manchester Derby?” Hali ya Man City inazidi kuongeza ugumu na ubora wa mechi hiyo kesho.
Kwa Man United, ndiyo wapo kwenye drip ya nafuu, wanaanza kuinuka, lakini ‘derby’ imewakuta mapema. Wana uwezo wa kuchagua, waitumie kuinuka au ndiyo wazame kabisa.
Msimamo bado unawashitaki kwa kuwa wako katika nafasi ya nane wakiwa na pointi 13, wameshinda mechi tatu tu katika tisa, wamepoteza mbili. Wakati Man City wako katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 17, wameshinda 5 na kupoteza mbili tu katika tisa.
Ukipita kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, mechi hiyo ya kesho tayari ni gumzo. Lakini mashabiki wengi wa Man United wana hofu, wanaona si kikosi kile cha enzi ya Alex Ferguson.
Kiasi fulani, sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea katika mechi iliyopita, kidogo inaamsha morali, kwamba huenda wakajaribu.
Ukweli, soka haiko hivyo na mechi ya watani, haipimwi kirahisi hivyo na mwisho, kikosi cha Man United, kadiri siku zinavyosonga, kinazidi kuwa kipana na inawezekana kikafanya vizuri kwenye mechi hiyo.
Nahodha wake, Wayne Rooney atakuwa anarejea uwanjani kutoka kwenye adhabu ya kadi nyekundu, usisahau katika mara zote 167 timu hizo zilizokutana kwenye michuano yote, Rooney ndiye mfungaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi, amepachika 11.
Giggs ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi, kapiga 36 lakini kesho atakuwa kwenye benchi katika nafasi ya kocha msaidizi.
Rekodi zinaonyesha Man United ndiyo wamekuwa wakiitawala zaidi mechi hiyo ya watani ingawa jibu la kesho haliwezi kuwa rahisi kama wengi wanavyotathmini.
Man United ina kikosi chenye wachezaji wengi wazoefu wa mechi kubwa kama Rooney, Radamel Falcao, Angel Di Maria, Robin van Persie, hakuna shaka kuwa wana uwezo wa kuwaangusha akina Kun Aguero, Yaya Toure, Vincent Kompany na wenzake. Yeyote anaweza kupoteza.
TAKWIMU:
MARA YA KWANZA:
Zilikutana Novemba 12, 1881 zikitumia majina ya West Gorton (Man City) 0–3 Newton Heath (Man United).
ZIMEKUTANA:
Mara       167
USHINDI:
Man United (69), Man City (48) na sare (50).
MECHI NYINGI:
Ryan Giggs (36)
MABAO MENGI:
 USHINDI MKUBWA:
United 1–6 City (1926)
United 0–5 City (1955)
United 5–0 City (1994)
United 1–6 City (2011).

Post a Comment

AddThis

 
Top