0


Kipa mkongwe wa Real Madrid, Iker Casillas amesema leo atabadilishana jezi na mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli lakini si wakati wa mapumziko.

Casillas amesema alipanga kufanya hivyo katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Anfield, lakini baada ya Balotelli kuingia matatizo baada ya kubadilishana jezi na Pepe, ikashindikana.
Casillas amesema atafanya hivyo leo wakati timu hizo zinakutana kwenye mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Dimba la Santiago Bernabeu.



Post a Comment

AddThis

 
Top