0

hii imetokea Indiana nchini Marekani ambapo Polisi waliisimamisha gari iliyokua na Waamerika weusi ndani yake ikiendeshwa na Mwanamke aitwae Lisa Mahone (47) akiwa na boyfriend wake Jamal Jones na watoto ambao ni Joseph wa miaka 14 na Janiya mwenye umri wa miaka 7 wakiwa kiti cha nyuma.

Baada ya Polisi kusimamisha gari walitaka Jamal aonyeshe kitambulisho chake lakini hakuwa nacho kwa wakati huo ambapo baadae walimtaka ashuke kutoka kwenye gari lakini Jamal akakataa ndipo Polisi wakaamua kuvunja kioo cha upande wa mlango alipokua amekaa Jamal na kumchukua.

Watoto wawili waliokua wamekaa nyuma ya gari waliumia baada ya kurukiwa na vipisi vya kioo kilichovujwa ambapo video ya tukio lote ilichukuliwa na mtoto Joseph aliekua amekaa kiti cha nyuma akiwa na mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 7 ambae ndio alilia sana baada ya Jamal kuvunjiwa kioo na kuchukuliwa.
Wakati huo wakilumbana na Jamal kumtaka ashuke, Lisa alikua kwenye simu akiwa amepiga 911 kuongea na Polisi akieleza kwamba yuko tayari kulipia fine ya kukutwa hajavaa mkanda ila kwa wakati huo alikua na haraka ya kuwahi hospitali ambako mama yake amelazwa na anakaribia kufariki.

Polisi waliohusika kwenye hili tukio wamesema walichukua maamuzi hayo pia baada ya kuona kulikua na hatari ya wao kushambuliwa sababu walimuona Jamal kama anajiandaa kufanya kitu flani walichohisi kinaweza kuwa ni kuwashambulia.



 Watu hawa wamefungua mashitaka kutokana na kitendo walichokiita ‘kuvuka mipaka kwa Polisi’ lakini Polisi kwa upande wao wamesema kisheria Polisi wanaruhusiwa kuuliza kitambulisho kwa abiria baada ya gari kusimamishwa na vilevile wanaruhusiwa kisheria kumwambia abiria atoke nje ya gari lake baada ya kusimamishwa kwa sababu ya usalama wao ‘Polisi’

 Polisi wamesema tukio zima lilichukua karibu dakika 13 ambapo kwenye sentensi nyingine baadhi ya watu wamelalamikia hiki kitendo na kuona kwamba ni muendelezo wa unyanyasaji kwa watu weusi nchini Marekani sababu pia Polisi walitumia bastola kumtisha Jamal japo hawakufyatua risasi yoyote.

Post a Comment

AddThis

 
Top