Tour ya Fiesta 2014 ilipita kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ambapo ripota wako wa nguvu Millard Ayo nilikua miongoni mwa watu walioenjoy sana kupita nayo mikoa mbalimbali na ikanipa nafasi ya kukaa zaidi na Wasanii wetu, kuwafahamu zaidi na kujua mengine ambayo nilikua siyajui mwanzoni.Miongoni mwa watu ambao nimegundua wana utani na utaenjoy kukaa nao ni pamoja na Fid Q, Mr. Blue, Baba Levo, Msechu na hayo ni baadhi tu lakini kuna wengine wana vituko vyao vya kipekee kama Raymond wa Tiptop Connection ambae mara nyingi huonekana kwenye stage na Madee ambapo wakati anamuigilizia Nay hakuwepo.
Raymond ambae pia ni mchekeshaji na mtani alionyesha uwezo wake kwenye kuigiza sauti ya Nay wa Mitego wakati Tour ya Fiesta ilipotua Mbeya (87.8 CloudsFM) ambapo ukishaisikiliza unaweza kuniachia comment yako kuniambia amempatia kwa asilimia ngapi?
Miongoni mwa wasanii ambao walichekeshwa sana na utundu huu wa Raymond ni pamoja na Mr. Blue, T.I.D, Linah, Linex na wengine ambao sauti zao wakicheka na kuongea zinasikika kwa mbali.
Home
»
» Unlabelled
» Hapa kuna dakika 1 ya Raymond wa Tiptop akimuigilizia Nay wa Mitego kuongea kwenye basi la Fiesta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment