0
Togo wametibua mipango ya Uganda kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuwachapa kwa bao 1-0 jijini Kampala, leo.

Lakini kama hiyo haitoshi, bao lililofungwa na Kokou Donou limeifanya The Cranes inayoongozwa na kocha wa zamani wa Yanga, Sredejovic Milutin ‘Micho’ na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kuingia kwenye kikosi cha Uganda kilichofungwa nyumbani baada ya miaka 10 kupita.
Mara ya mwisho, Uganda ilipoteza nyumbani kwenye michuano ya Caf mwaka 2004.
Kipigo hicho, kimeiyumbisha Uganda ambayo ilikuwa na mwendo mzuri.
Matokeo mengine ya leo ya michuano ya kuwania kucheza Kombe la Mataida Afrika ni haya.
Niger 0-0 Zambia
Msumbiji 2-0 Cape Verde
DR Congo 1-2 Ivory Coast
Gabon 2-0 Burkina Faso
Sierra Leone 0-0 Cameroon

Ethiopia 0-Mali 2

Post a Comment

AddThis

 
Top