0



Miaka 25 Sasa tokea Afariki Dunia Guiji wa Muziki wa Rumba FRANCO LUAMBO MAKIADI.
Ingawa Mengi yamesha andikwa kwa kumhenzi GRAND MAITRE FRANCO, Leo hii nachukua fursa ya kuchambua Baadhi ya Nyimbo zake zilizo pigwa Marufuku.
Wala sio Siri tunapo tamka ya kwamba ” GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI FRANCO ” katokea kua Tajiri sana katika kipindi cha Utawala wa Rais MOBUTU SESESEKO.
Mbali na Urafiki ambao FRANCO LUAMBO alikuanao na RAIS MOBUTU, ilifikia wakati fulani Serekali ikazipiga marufuku Baadhi ya Nyimbo zake zilizo kua na Ujumbe uliokeuka Maadili ya Umma.
Kutokana pia na Sababu mbali mbali, SEREKALI YA RAIS MOBUTU, ilikua makini sana na Wanamuziki, hasa palikua na Watu hodari ambao kazi yao kuu ilikua kufanya uchunguzi wakina kwa Ujumbe unao patikana kwenye NYIMBO. Ikiwa kwa Namna moja au Nyingine kwenye Wimbo wewe Msanii ukithubutu Kutamka Jina la Mpinzani, Basi Wimbo huo kamwe hauta ruhusiwa na Wewe mwenyewe utajikuta ukiwa matatani.
1. Mkasa kama huo umemkuta  TABU LEY ROCHEREAU, wakati katunga Wimbo ” KASHAMA NKOYI ” kwenye Wimbo huo, ROCHEREAU kayatamka Maneno haya : ” Boni Oweleli, Okende liboso ya Baninga, Soki okutani na LUMUMBA okoloba nini PAPA ?  Tokengelaki yoo te  KASHAMA  NKOYI / INAKUAJE UKASAFIRI, WATUTANGULIA SISI WENZIO, HUKO UENDAKO, UTAKAPO KUTANA NA LUMUMBA UTAMWAMBIAJE BABA ? WALA HATUJAWAHI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KWA YALE YALIYO KUKUTA ” KASHAMA NKOYI “.
Wimbo umepigwa Marufuku, sio kwasababu  Katajwa LUMUMBA hapana, Bali Jina ” KASHAMA NKOYI “, Serekali ya MOBUTU yamushutumu ROCHEREAU TABU LEY kutumia Jina hilo Bandia kwakumhenzi ” PIERRE MULELE ” ambae alikua Mmoja kati ya MAWAZIRI wa EMERY PATRICE LUMUMBA,SHUJAA WA UHURU WA CONGO. Baada ya kuuwawa LUMUMBA, PIERRE MULELE kasimama kidete kupambana na SEREKALI ya MOBUTU. Vikosi vya Waasi vilio tawala mashariki mwa Congo hasa kwenye Mikoa ya KIVU. VIlikua vikimchukulia yeye kama Kiongozi wao Mkuu. Ndiko katokea LAURENT DESIRE KABILA. PIERRE MULELE kauwawa Mwaka 1968.
2. FRANCO LUAMBO NA WIMBO WAKE ” LUVUMBU NDOKI “, Kwenye Wimbo huo, FRANCO kaimba kwa KIKONGO, Lugha yake ya Asili. Ujumbe kwenye Wimbo huo ni kwamba ” WEWE LUVUMBU MTU AMBAE KIJIJI KIZIMA KINAKUTEGEMEA, WANAKIJIJI WOTE WAKO CHINI YA USIMAMIZI WAKO, KUTOKANA NA UCHAWI WAKO, UMEWAMALIZA NDUGU ZAKO WOTE WAKIKE KAMAVILE WAKIUME, SASA WAKATI UTAKAPO FARIKI, NANI YULE ATAKAE KUZIKA ? MIMI FRANÇOIS NASHINDWA KABISA KULIA, KWAKWELI HUA NAJIULIZA, KWANI UCHAWI WAKO UPO MGONGONI AU TUMBONI MWAKO.
Wimbo huo Ulipigwa marufuku paletuu ulipo tolewa, SEREKALI ya RAIS MOBUTU, yasema kwamba, Kupitia Wimbo huo, FRANCO LUAMBO MAKIADI kawatukuza Wanasiasa Wanne Walio Uwawa kwa Kunyongwa kwa Madai kwamba walikua na nia ya kuipindua Serekali Mwaka 1966.  Wanasiasa hao walio nyongwa ni hawa :
1. JÉRÔME ANANY ( WAZIRI WA ZAMANI WA ULINZI WA TAIFA )
2. EMMANUEL BAMBA ( SENETA )
3. ÉVARISTE KIMBA ( WAZIRI MKUU WA ZAMANI )
4. ALEXANDRE MAHAMBA ( WAZIRI WA ARDHI )
Baada ya Wimbo huo kutolewa, FRANCO LUAMBO  Tetesi zilimjia kana kwamba SEREKALI ipo kwenye harakati ya kumfungulia Mashitaka na Kumuweka Jela. LUAMBO kavuka yeye pamoja na Group lake nakwenda kujihifadhi kwa Mda JIJINI BRAZZAVILLE.
Akiwa JIJINI BRAZZAVILLE, RAIS MOBUTU kamtumia Wajumbe na kumshawishi arudi KINSHASA, maisha yake haitakua hatarini. FRANCO LUAMBO kaupokea wito huo ila kawa katika hali ya Mtu mwenye Kusita. Mwishowe kaamua kurudi KINSHASA.
Akiwa JIJINI KINSHASA, FRANCO LUAMBO kajikuta yuko matatani, Kakaribishwa na kikosi cha Wanajeshi. Wakamuamuru yeye na Group lake wapande ndani ya Gari lao, nakupelekwa moja kwa moja  Jela ya NDOLO. Huko walikaa kwa Mda wa Siku Mbili, yasemekana Walicharazwa bakora sawasawa,
Baada yakutolewa kwenye Jela ya NDOLO,  FRANCO LUAMBO na Group lake, wakahamishwa kwenye Kambi ya Jeshi ” TSHATSHI “. Huko pia wakashikiliwa kwa siku kadhaa wakiwa kambini humo.
Ndipo Ikatokea Siku amabayo RAIS MOBUTU akaja mwenyewe kujadiliana na LUAMBO MAKIADI. kamtamkia Maneno haya : ( KUANZIA LEO HII HADI ITAKAPO FIKIA WAKATI WA MIMI KUONDOKA MADARAKANI, UTAKUA UKINIIMBIA MIMI, WATAKIWA KUNIFANYIA KAZI ZANGU ZOTE, NA TENA KWA WAKATI WOWOTE NTAKAO KUHITAJI ) .
Nakwakeli Tokea siku hiyo, FRANCO LUAMBO kawa kiungo kikuu sana kwa Kampeni ya RAIS MOBUTU. na kutokana na ushirikiano huo, kanufaika sana kuwazidi Wanamuziki wengine wote wa Inchi hiyo katika kipindi hicho cha utawala wa Serekali ya MOBUTU SESESEKO KUKU NGBWENDU WAZABANGA JOSEPH DESIRE.
Mwaka 1978,  FRANCO LUAMBO MAKIADI kawekwa tena JELA kutokana na Utunzi wa Nyimbo ( HELEINI na JACKIE ),
Nyimbo mbili hizo zilikua na Maneno machafu sana tena yaku yaharibu maadili ya Umma. Sheria ikachukuliwa kuzipiga Marufuku zisipitishwe kwenye Radio na TV ya taifa. FRANCO mwenyewe kajitetea, kasema wala NYIMBO hizo hajizauzwa Sokoni zilikua bado hazijawekwa kwenye CD. bali Watu walikua wakizisikiliza Wakati wa SHOO kwenye Ukumbi wake wa 1.2.3 KINSHASA.
Aliekua MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI kipindi hicho  ” Mr  LEON KENGO WA DONDO “,kalisimamia swala hilo, nakuamuru FRANCO LUAMBO awekwe Jela, kapelekwa kwenye JELA ya ” LUZUBU ” inayo patikana kwenye MKOA WA BAS CONGO aliko zaliwa FRANCO.
Huko JELA, FRANCO kawa mwenye masikitiko, Kwanini RAIS MOBUTU kashindwa kumsaidia ? yeye ambae alikua akimchukulia kama Rafiki. FRANCO kapigwa na Ugonjwa wa HEMORRHOID. katabaanika kabisa. Kabaki na chuki na kinyongo dhidi ya MWANASHERIA ” LEON KENGO WA DONDO ” aliempeleka JELA. Haelewi kwanini kawekwa kizuizini wakati Hajawahi kuzidumbwiza Nyimbo hizo hadharani.
Miaka michache baadae, palitokea na mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, LEON KENGO WA DONDO  Kanenguliwa Cheo cha MWANA SHERIA MKUU WA SEREKALI na kutomwa JIJINI BRUSSELS kama BALOZI WA CONGO.
Furaha ilikuaje kwa FRANCO LUAMBO MAKIADI ?, bila kukawia kamtungia Wimbo ” TAILLEUR ” kwenye Wimbo huo FRANCO kanena haya : ( LIKAMBO NALOBAKI LOBI, MONOKO NA NGAI NGANGA / UTABIRI WANGU WATOKEA KUA KWELI, MDOMO WANGU KAMA WA MGANGA WA JADI ).
MOKOLO TONGA ABOTOLI TONGA OKOTONGA NANI ? / MWENYE SINDANO YAKE KESHA ICHUKUA, SASA UTATUMIA NINI ILIUENDELEE KUWACHOMA WENGINE?
OLOBAKI TROP NA ESIKA YANGOO BATIE YO PEMBENI LOBA LISUSU MAMA / ULIKUA UKIKIJIVUNIA SANA CHEO HICHO, SIUMEONA WAMEKUONDOA, UNANINI CHAKUONGEA? Wimbo huo pia ukapigwa Marufuku kwa Mda.
Mwaka 1982, RAIS MOBUTU Kamwitisha LEON KENGO WA DONDO , na kamteua kama WAZIRI MKUU WA INCHI.
FRANCO LUAMBO hajaridhishwa ni kitendo cha RAIS MOBUTU kumpa KENGO WA DONDO cheo cha WAZIRI MKUU, bila kusita Katunga Wimbo ” TRES FACHE “. Mtamsikia akiiimba : ( OKOSI NGAI MAMA YONAYE BOBOYANA, LOBI LISUSU BAKUTI YO NA VOITURE NA YEE, ELOKO NASALA NAYEBI TEEOO MOKILI / WANIDANGANYA KAMA NYIE WAWILI SIO TENA MARAFIKI, KESHO YAKE WATU WAMEWAONA MKIWA PAMOJA NDANI YA GARI, JAMANI KOSA GANI NILILOLIFANYA MIE!!! ). Kadhalika Wimbo huo Ulipigwa pia Marufuku.
GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI KAFARIKI DUNIA  INCHINI BELGIUM TAREHE  12-10-1989.
SIKU YA MAZISHI YAKE, LEON KENGO WA DONDO AMBAE NDIE ALIEKUA WAZIRI MKUU, KAJA KUTOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA NIABA YA SEREKALI.
WAKATI WA MISA  YA MAZISHI YAKE, PADRE KASEMA : ” LUAMBO ALIKUA MTUME WA MUZIKI, HAKUNA ALICHOKISAHAU KATIKA UTUNZI WAKE, KAVICHAMBUA VITU KADHALIKA NA WATU WAKILA RIKA, HATA RAIS MOBUTU HAJAACHWA NYUMA.
NYIMBO ZAKE KADHAA ZILIPIGWA MARUFUKU, HATA HIVYO ZILIENDELEA KUPENDWA SANA NA UMMA. HUKU NYIMBO ZAKE  NYINGINE HADI LEO HUCHUKULIWA KAMA NEMBO YA TAIFA.

Post a Comment

AddThis

 
Top