Klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani imeendelea na rekodi nzuri ya mwanzo mzuri wa ligi kwa kushinda mechi zake zote tatu za mwanzo.
Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Manungu, Mtibwa Sugar leo imefanikiwa kushika uongozi wa ligi na kuiengua Azam FC baada ya kuifunga JKT Mgambo kwa 1-0.
Mtibwa ambayo mechi yake ya kwanza iliiadhibu Yanga 2-0, kabla ya kuwakandamiza ‘Wazee wa kukatiza mapori’ Ndanda FC 3-1, sasa imefikisha jumla ya pointi 9 katika msimamo wa ligi Vodacom Premier League.
Goli la Mtibwa Sugar leo lilifungwa na mchezaji Ally Shomari dakika 10 baada ya mchezo kuanza
Post a Comment