0



Siku chache baada ya Ndanda FC kumtupia virago kocha wake, Denis Kitambi, makocha wanne wamejitokeza kuomba kazi ya kuifundisha timu hiyo akiwemo Mkenya mmoja.

Ndanda wameamua kuachana na Kitambi  kufuatia kufanya vibaya katika mechi tatu mfululizo kwa kufungwa hivyo kujikuta ikiwa katika nafasi ya 12 ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi tatu licha ya kuanza kwa kishindo katika mchezo wa kwanza kwa kuifunga Stand United mabao 4-1.

Katibu wa Ndanda, Seleman Kachele, amesema makocha wanne hadi sasa wamejitokeza kuomba kuifundisha timu hiyo kwenye ligi  huku wakitarajia kupokea CV za makocha zaidi na kudai kuwa wapo katika mazungumzo nao ili kuweza kupata yule atakayefaa kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.

Aidha, katibu huyo alieleza kuwa kwa sasa timu hiyo ipo chini ya mkurugenzi wa ufundi wa Ndanda, Amini Mawazo hadi hapo atakapopatikana kocha mpya wa kuiongoza.
“Kuna makocha wanne ambao wameleta barua zao za kuomba kuifundisha Ndanda watatu kutoka ndani ya nchi na mmoja kutoka Kenya.
“Tunaendelea kufanya nao mazungumzo na wote wana leseni za Class A, hivyo ni matarajio yetu tutapata kocha mzuri wa kuifundisha timu yetu kwani lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vyema kwenye ligi.

“Muda si mrefu tutamtangaza kocha mpya mara baada ya kukubaliana naye,” alisema Kitambi.

Post a Comment

AddThis

 
Top