0

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, hatimaye Kocha maarufu nchini, Sylvestre Marsh amerejea mzigoni.

SALEHJEMBE limemshuhudia Marsh akiwanoa vijana na watoto wadogo katika timu ya ya watoto iliyo chini yake.
Kocha huyo aliumwa kwa kipindi kirefu na kulazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar, lakini sasa hali yake ni nzuri na amezidi kuonyesha mapenzi kwa vijana na watoto ambao amekuwa akiwafundisha kwa kujitolea.

Marsh alifanya mazungumzo na watoto hao ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo kwa maelezo na badaye kinadharia.
Watoto mchanganyiko, wa kike na kiume walikuwa wakishiriki mafunzo ya kocha huyo wa zamani wa timu za taifa za vijana pamoja na ile ya wakubwa.

Post a Comment

AddThis

 
Top