0


likutana na nahodha wa zamani wa Simba SC, Abdul Mashine na kufanya naye mahojiano marefu. Kuelekea mchezo wa mahasimu wa soka la Tanzania, Yanga SC dhidi ya Simba mwisho wa wiki hii, bila shaka mpenzi msomaji wa mtandao huu utapata mengi muhimu ambayo kama ‘ mtu wa soka’ ungependa kuyafahamu kutoka kwa wachezaji walioshiriki moja kwa moja katika mchezo huo mkubwa zaidi Afrika Mashariki ‘
Shaffihdauda.com – Mashine, kuelekea mchezo wa Simba na Yanga, matokeo ya mechi za nyuma huwa yana maana sana. Ukitazama Simba haijapata ushindi katika michezo mitatu iliyocheza, Yanga wameshinda mara mbili na kupoteza mara moja.

“Matokeo ya mechi ya Yanga unaweza kuyaona baada ya dakika 90. Yanga ambao wanapnekana ni wazuri, wanacheza kitimu huku wakiwa na matokeo ya ushindi katika mechi mechi mbili zilizopita, unaweza kuwakataa. Ukashangaa!, ukajisemea ‘ Simba leo wametokea wapi ?’. Yanga wanaweza ‘ kukamatwa uwanjani na kuwafanya watu wengi kuwa na maswali na kiwango cha Simba. Yanga dhidi ya Simba isitazamwe kwa ‘ jicho la kawaida’ ni mechi kubwa ambayo inatakiwa kuitwa ‘ Yanga na Simba’huwa mechi isiyotazama matokeo yaliyopita.“

 Simba na Yanga zilifungana mabao 3-3 mwaka uliopita. Simba walitanguliwa kwa mabao 3-0, lakini katika nusu ya pili ya mchezo Simba walisawazisha mabao yote na kutengeneza sare ya mabao 3-3 baada ya kumalizika kwa dakika 90. Kitu ambacho kilizungumzwa sana na wachezaji wa Simba, ambacho Mwalimu ‘ King’ ( Abdallah Kibadeni) alikisema wakati wa mapumziko ni kwa; – ‘Ninafahamu tuna timu mbili kati yetu’, kwa maana kwa alimaanisha wapo wachezaji ambao walicheza mchezo ule huku wakijihusisha na upande mmoja wa mgogoro wa timu, upande mwingine wakicheza kulikuwa na wachezaji ‘ watiifu’ ambao walikuwa uwanjani kucheza mpira huku wakiongozwa na mbinu za benchi la ufundi, na akili zao binafsi ili kuisaidia timu. King alifanya mabadiliko mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na aliwaambia wachezaji; ‘ Nendeni mkacheze mpira’.
 

Kama mchezaji-nahodha wa zamani wa Simba ambaye umeshiriki katika michezo ya mahasimu hao wa soka nchini, Simba na Yanga, Je huwa kuna kundi ndani ya Simba ambalo linaweza kuwa linataka kuona timu yao ikifungwa na Yanga kwa maslahi yao. Tunaizungumzia zaidi, Simba kwa sababu ni mchezaji uliyepata kucheza hapo na kupata mafanikio. Je, kauli ya ‘ timu mbili’ ambayo aliitoa, King msimu uliopita ilimaanisha nini?.

Simba walikomboa mabao yote lakini upande wa pili, nikimaanisha Yanga kuna wachezaji ambao hawajakuwa na mahusiano mazuri na baadhi ya viongozi huku wengine wakiwa hawajapangwa katika mchezo wowote hadi sasa, Unaweza kuzungumza kuhusu Simba lakini vipi upande wa Yanga pia huwa kuna makundi ambayo yanataka Yanga yenyewe ifungwe?. Ni presha ya wachezaji ndiyo inayoleta matokeo ya ‘ kusimumua’?

ABDUL MASHINE…….ANAJIBU YOTE HAYO
“ Mechi ya Simba na Yanga huwa na presha kubwa sana. Nakumbuka wakati nikiwa mchezaji wa Simba kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wachezaji wengine walikuwa wakishindwa kula chakula cha mchana. Simaanishi kuwa chakula hakikuwepo, hapana, chakula kipo. Mchezaji unachukua chakula chako na kwenda katika chu,ba chako lakini anashindwa kula kutokana na ‘ presha ya mechi’. Unaweza kwenda katika chumba na mchezaji mwenzako ili kumletea masihara ( utani) ambao mmekuwa nao siku zote, lakini unaweza kushangaa na kile anachoweza kukujibu. Yote sababu ya presha ya Simba na Yanga. Mechi itakuwaje, mechi itakwishaje?. Kila mmoja anakuwa bize na mawazo ya mechi, wengine humuomba Mungu ili mechi imalizike kwa usalama lakini mwingine anakuwa akijiombea Mungu yeye binafsi mechi imalizike salama kwa upande wake. Cha pili mchezaji huomba ushindi kwa timu yake. Presha ya mechi huondolewa na mchezaji mwenyewe kama anajitaji kufanya hivyo, ukiikubali itakuwa shida kufanya vizuri. Wingi wa watu, jinsi ya kucheza mbele yao inakuwa ni vigumu, sababu mashabiki hupagawisha siku ya mechi ya Simba na Yanga. Mchezaji hukisahau yote na kuamua kutekeleza yale uliyoagizwa itakuwa vizuri kufanya vizuri, hata kama matokeo hayatakuwa mazuri. “
“ Simba walianza vibaya katika mechi ya msimu uliopita kutokana na presha waliyokuwa nayo wachezaji, lakini hali hiyo ilihamia upande wa Yanga baada ya Simba kujihamini na kuwafanya Yanga kuwa kwenye presha. Suala la uwepo wa ‘ timu mbili’ katika kikosi kimoja lipo, ila linaweza kuwa la kihisia zaidi kwa sababu wakati mimi nikiwa mchezaji. ( akikimbushia mechi ambayo Simba iliifunga Yanga mwaka 1993, bao la Dua Said) kuna mchezaji ambaye alihusishishwa moja kwa moja bila uthibitisho kuwa alikuwa amenunuliwa na upande wa pili na usiku kuelekea siku ya mchezo mchezaji huyo alikuwa,”
……… Unajua nini kiliendelea, endelea kufuatilia mfululizo wa mahojiano haya na nahodha huyo wa zamani wa Simba , Abdul Mashine….

Post a Comment

AddThis

 
Top