0
CHEKA (KATIKATI) AKIWA NA WAANDISHI WA GAZETI LA CHAMPIONI, SALEH ALLY NA JOHN JOSEPH.

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘SMG’, ameibuka na kusema kuwa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro ndiyo itaibuka bingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara kutokana na ushindani inaouonyesha kwa timu inazokutana nazo.

Mtibwa imeanza vizuri ligi kwa kuzifunga Yanga, Ndanda na Mgambo JKT, kesho Jumamosi inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuivaa Polisi Morogoro ambao wamekuwa wakiwasumbua kwa muda mrefu.
“Ndoto yangu ni kuona Mtibwa wanakuwa mabingwa wa msimu huu, kwani naamini itakuwa ni zawadi kwetu watu wa Morogoro kwa sababu hata usajili wao wameufanya kwa umakini mkubwa, ndiyo maana kila wanayekutana naye lazima wamfunge,” alisema Cheka.
Mtibwa imekuwa ikishinda mfululizo tokea kuanza kwa ligi hiyo. Mechi yake ya kwanza iliyokuwa ya ufunguzi wa ligi ilitoa kipigo kwa Yanga cha mabao 2-0.

Post a Comment

AddThis

 
Top