0


Mshambulizi, Ahmed Musa alifunga mabao mawili wakati, Nigeria ilijitutumua na kuishinda ‘ timu inayowasumbua kila mara, Sudan Kaskazini’ katika mchezo wa kundi A kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, baadae mwaka ujao nchini, Morocco. Nigeria ilipoteza mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini, Khartoon lakini walicheza kwa nguvu mara baada ya Salah Ibrahim kuwasawazishia wageni katika dakika ya 56 , akifuta bao la dakika ya 48 la Musa.

Mechi hiyo ambayo ilishuhudia kipindi cha kwanza kutotoa bao lolote ilikuwa kali katika dakika 45 za kipindi cha pili. Aaron Samuel aliifungia ‘ Super Eagle’ bao la pili dakika kumi baada ya Salah kusawazisha. Musa akafunga bao la tatu dakika ya 87 na kuwahakikishia mabingwa hao wa Afrika ushindi wa kwanza katika kundi. Vinara wa kundi hilo, Afrika Kusini walivutwa shati wakicheza nyumbani dhidi ya timu ngumu ya Congo Brazaville. Bafana Bafana bado wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi nane, moja zaidi ya Congo.

Nigeria imefikisha pointi nne katika nafasi ya tatu, Sudan wanaburuza mkia zikiwa zimebaki mechi mbili kwa kila timu. Timu mbili za juu zitafuzu moja kwa moja kwa fainali hizo ambazo zitafanyika, Nchini, Morocco, 2015. Timu zote nne kimahesabu zina uwezo wa kufuzu kutoka katika kundi hilo. Congo wataikaribisha, Nigeria jijini, Brazaville katikati ya mwezi ujao na mchezo huo unaweza kutoa mwangaza ipi timu itakayofuzu na kuungana na Afrika Kusini watakaocheza nyumbani na Sudan katika uwanja wa nyumbani. Afrika Kusini wanahitaji pointi tatu tu ili wafuzu kwa fainali za mwakani.

Post a Comment

AddThis

 
Top