0





TUNAJITAHIDI KILA WIKI KUWALETEA HISTORIA YA WASANII AMBAO KWA LEO HII HAWAKO TENA KWENYE DUNIA HII!!!


WIKI HII TUNAMKUMBUKA MAMA ABETI MASIKINI.BAADA YA TAKRIBAN MIAKA 20 TOKEA PALE ALIPO FARIKI JIJINI PARIS ( VILLEJUIF ) TAREHE 28-09-1994.

Jina lake kamili ni ” ELISABETH FINANT ” ,Kazaliwa Tarehe 09-11-1954 MJINI KISANGANI Mashariki mwa INCHI YA CONGO. Katokea kwenye Familia Tajiri ya Watoto 8.

Baba yake Mzazi MZEE ” JEAN FINANT ” alikua chotara, Mchanganyiko wa Mkongomani na Mbeljiji.
Mwaka 1961, Baba yake kauwawa kikatili MJINI MBUJIMAYI, kutokana na matatizo ya kisiasa, MR FINANT alikua Mwanachama wa MLC, Chama cha hayati EMERY PATRICE LUMUMBA, Waziri Mkuu wa zamani Inchini CONGO Ambae pia ndie Shujaa wa Uhuru wa Inchi hiyo !!!.

Hali hiyo ikampelekea Mama yake ABETI MASIKINI, kuchukua uamuzi wa kuhamia JIJINI KINSHASA ili apate kujihifadhi akiwa na Wanae.
JIJINI KINSHASA, ABETI MASIKINI karudi darasani kwenye Shule iliokua ikijulikana kwa Jina la ” LYCÉE SACRE CŒUR ” kwa sasa inaitwa ” BOSANGANI “.

Baada ya kumaliza shule ya sekondari, ABETI MASIKINI kaajiriwa kama KATIBU kwenye ofisi ya Waziri wa Utamaduni Mheshimiwa PIERRE MUSHETE.
Kwamshangao wandugu zake na Familia, ABETI MASIKINI kaamua kujiuzuru kwenye Kazi aliokua nayo, na kuambatana na Fani ya Muziki na Ndipo kajipachika Jina la BETTY.

Mwaka 1971 Chini ya Usimamizi wa Mwanamuziki ” GERARD MADIATA “, palikuwepo na Mashindano ya kumtafuta Mwanamuziki Chipukizi, na ABETI MASIKINI kaamua kushiriki kwenye mashindano hayo, Kwa bahati mbaya hajafaulu, katoka wa tatu.

Ndo kwanza niayake yakuupenda Muziki ikzidi kuchipukia, Huku akiwa bado Mtoto Mdogo wa Miaka 17, na iliapate kuruhusiwa kudumbwiza SHOO kwa Jina lake mwenyewe, ilibidi ajiongezee Miaka Mitatu zaidi akawa anasema yeye ni Mkubwa wa miaka 20.

Akisaidiwa na Kaka yake ” JEAN ABUMBA ” Ambae ni Mpiga Gita mashuhuri, ABETI MASIKINI akawa kila siku anafanya SHOO kwenye Vilabu vidogodogo JIJINI KINSHASA.

MAISHA YAKE YA NDOA
MAMA ABETI MASIKINI kaishi maisha ya kimahaba na MR GERARD AKUESON, Raia kutoka Inchi ya TOGO, ambae ndie aliekua MENEJA wake Mkuu.Tokea Mwaka 1972 hadi ilipofikia Mwaka 1989 ndopo wakaja kufunga Ndoa JIJINI PARIS. ABETI MASIKINI kaacha Watoto Wanne, Wakike 3 na Mvulana 1.

KAZI YAKE YA MUZIKI

ABETI MASIKINI Kakutana na MR GERARD AKUESON JIJINI KINSHASA, Mwaka 1971, Tutasema tokea Mwaka huo ndo career yake ya Muziki ilipo anza rasmi.
MENEJA wake huyo, Kamshauri waongozane na kuhamia kwenye Inchi za WEST AFRICA, ambako kaona atapata mafaanikio zaidi. Wala ABETI MASIKINI hajasita kwa pendekezo hilo,ndipo walivyo hamia huko na kwakweli kajikuta akiwa na Mashabiki wengi sana kwenye Inchi za BENIN, COTE D’IVOIRE, TOGO, NIGER, GUINEA,NIGERIA, GHANA..

Baada ya Miaka kadhaa akiwa kwenye Inchi za WEST AFRICA, ABETI MASIKINI kaamua kurudi Inchini CONGO, mapokezi Inchi kwao hayakua mazuri, Watu wengi walikua hawamfahamu kabisa,na kilicho mponza zaidi nikuona kwa kipindi hicho alikua hajaweka hata na Album moja Sokoni.
Hata hivyo, Kaamua kufanya SHOO JIJINI KINSHASA kwenye Ukumbi wa CINE PALLADIUM, kama ilivyo tarajiwa, Watu 12 pekee ndio walio jitokeza.

Wala ABETI MASIKI hajavunjika moyo kwa matokea hayo, ndo kwanza kaendelea kufanya kazi kwa bidii ili malengo yake yakamilike. Kaanza kufanya mazoezi ya kuboresha Sauti yake,
Mwaka 1973 katoa Album yake ya kwanza ( PIERRE CARDIN ) ikiwa na Nyimbo kadhaa zikiwemo : ( Mutoto Wangu, Bibile, Aziza, Miwela, Safariet Papy Yaka ).

Album hii haijapokelewa vilivyo nawakazi wa JIJI LA KINSHASA, Machoni mwao humchukulia ABETI MASIKINI kama Mgeni, na hasa wamemlaumu kwa Tabia yake yakupenda kuimba baadhi ya nyimbo zake kwa Lugha ya KISWAHILI.

Mchapa kazi alivyokua, ABETI MASIKINI kapatwa na wazo lakuunda Group lake nakalipa jina la ” LES REDOUTABLES “, akiwa na Wanenguaji wake machachari walio julikana kama ” LES TIGRESSES “. hilo likafanya Watu wengi waanze kuvutiwa naye.

SHOO zake JIJINI KINSHASA zikawa gumzo, Kazi aliokua akifanya MENEJA wake pia ikazaa matunda mema, kafaanikiwa kupata Mkataba utakao mpeleka ABETI MASIKINI  kwenda kufanya SHOO kwenye Ukumbi wa OLYMPIA JIJINI PARIS Mwaka 1973.

Akiwa Njiani kuelekea JIJINI PARIS kwenye SHOO ya OLYMPIA, katua JIJINI DAKAR( SENEGAL ) ambako kafanya SHOO ilioudhuriwa na Rais wa zamani wa Inchi hiyo ” LEOPOLD SEDAR SENGHOR “. Pesa zilizo tokana na SHOO hiyo, ABETI MASIKINI kazitoa kama Msaada kwa Watu waliopigwa na Shida ya Ukame wa Ardhi.

Tarehe 19-02-1973, ABETI MASIKINI kafanya SHOO nzuri iliowavutia hasa mashabiki wakizungu kwenye Ukumbi wa OLYMPIA JIJINI PARIS.

Tarehe 19-06-1974, ABETI MASIKINI kafaanikiwa kufanya SHOO kabambe Inchini AMERICA JIJINI NEW YORK kwenye Ukumbi wa ” CARNEGIE HALL “
Mwaka 1974 ,Umaarufu wake ulizidi kuja juu zaidi pale alipopewa fursa ya kudumbwiza na kuchangia jukwaa kwa pamoja na JAMES BROWN, MYRIAM MAKEBA, TABU LEY, FRANCO LUAMBO MAKIADI, kabla ya pambano la Masumbwi lakihistoria kati ya MOHAMED ALI na GEORGE FOREMAN JIJINI KINSHASA.

Mwaka 1975 Katoa Album yake ya pili ” LA VOIX DU ZAIRE “, Mnanyimbo nzuri kama hizi : Likayabo,Yamba yamba? Kiliki, Bamba, Nalikupenda, Ngoyaye Belle Bellow …”
Mwaka huo 1975, ABETI MASIKINI kapokea mualiko kutoka kwa ” BRUNO COQUATRIX ” ambae ndie Mmiliki wa Ukumbi wa OLYMPIA JIJINI PARIS, nakaenda kufanya SHOO kwa Siku mbili mfululizo. Ndipo kapachikwa jina la ” TIGER MWENYE KUCHA ZA DHAHABU “.

Mwaka 1976, Mwaka huo ulikua mgumu kwa ABETI MASIKINI, kajikuta kampata mpinzani wauhakika,naye si mwengine bali ni MAMA MPONGO LOVE, ambae kaja Juu kabisa nakuongoza HIT PARADE kwenye Radio ya Taifa ya CONGO. Wimbo wake ” PAS POSSIBLE ” ukiwa mwenye kupendwa sana!!!

Mwaka 1977, Lilitokea Tukio Kuu nihasa pale ABETI MASIKINI na MPONGO LOVE walivyo amua kufanya SHOO kwa pamoja kwenye Ukumbi wa ” CINE PALLADIUM ” JIJINI KINSHASA, SHOO hiyo iliacha hadithi kwakua kila mmoja wao kaimba kiaina yake, Akina Mama hao waliweka Misingi Mema kwa Wanamuziki wa Kike wakizazi kijacho.

ABETI MASIKINI ataendelea kukumbukwa daima kwakua yeye ni Darasa tosha, Wanamuziki Maarufu wamepitia kwenye ORCHESTRA YAKE, Ntawataja :  Mbilia Bel (Mnenguaji 1976 -1981), Lokua Kanza (guitarist 1980-81), Abby Surya (Mnenguaji 1984-1986), Malage De Lugendo (chorist), Tshala Muana (Mnenguaji 1978-79), Yondo Sister(Mnenguaji Mwaka 1986), Lambio Lambio (Mnenguaji), Komba Bellow(percussionnist), Richard Shomari (chorist), Joëlle Esso (Mnenguaji), …

ABETI MASIKINI ni Mmoja kati ya Wanamuziki wa Kike barani Africa ambao wamefaanikiwa kujiwekea Jina Kimataifa, Ni Mwanamke aliedhihirisha Kipaji chake na kufahamika Inchini Congo, Inchi ambayo MUZIKI hutawalia na  Wanaume. ABETI MASIKINI Alikua pia Mpigania haki ya Wanawake.

DISCOGRAPHY
Albums
  • 1973 : Pierre Cardin présente Abeti (Les Disques Pierre Cardin/ Sonafric) Ref: SAF 93501
  • 1975 : La voix du Zaire, l’idole de l’Afrique (Pathé Marconi/EMI) Ref: 2C O64 15741
  • 1976 : Abeti à Paris (Pathé Marconi/EMI) Ref: 2C06215.772
  • 1977 : Abeti (Capriccio) Ref: 37014
  • 1977 : Visages (BBZ productions/RCA) Ref: BZL 7014
  • 1978 : Abeti: Kupepe Suka (BBZ productions/RCA) Ref: BZL 7019, RCA – BZL 7019
  • 1979 : Na Pesi Yo Mboté (45 tours)
  • 1979 : Bifamuri (45 tours)
  • 1979 : Mbanda Na Ngai (45 tours)
  • 1980 : Mokomboso (Eddy’son/ Disques Sonics)) Ref: 79398 / 79398
  • 1981 : Dixième anniversaire (Dragon Phénix) Ref: DPX 829
  • 1982 : Abeti (Iris production) Ref: IRS 001
  • 1983 : Abeti: Naleli (Zika Production)
  • 1984 : Amour Ya Sens Unique (IAD/ Industrie Africaine du Disque) Ref:IAD/S 0015
  • 1984 : Abeti & Eyenga Moseka : Le Duo Du Siècle (IAD/ Industrie Africaine du Disque) Ref: IAD/S 0016
  • 1985 : Ba Mauvais Copiste (Win Records/Africa New Sound/Tabansi) Ref: WNL 403, ANS 8402
  • 1985 : Samoura (Bade Stars Music) Ref: AM 030
  • 1986 : Je Suis Fâché (Bade Stars Music) Ref: AM 033
  • 1987 : En colère (Bade Stars Music) Ref: AM 035
  • 1988 : Scandale De Jalousie (maxi 45 tours) (Polygram/ LAB) Ref: LAB 101
  • 1990 : La Reine du soukous (AMG/Polygram)

SHOO KABAMBE ALIZO ZIFANYA ABETI MASIKINI :

FILAMU ZAKE NA VIDEO

  • 1978 : Abeti in Holland (Radio Netherlands)
  • 1988 : Abeti au Zenith (VHS) (Jimmy International)
  • 2008 : Best of clips (DVD) (Akueson World Wide)
  • 2008 : Soul Power de Jeffrey Levy-Hinte (DVD bonus) (Océan Films)
  • 2014 : Abeti Masikini, Le Combat d’une Femme de Laura Kutila et Ne Kunda Nlaba (Labson Bizizi/ Ciné Kongo Ltd)

Post a Comment

AddThis

 
Top