MOJA ya tatizo kubwa linalowasumbua wasanii wetu, hasa hawa wa muziki wa kizazi kipya, ni ukosefu wa usimamizi makini wa kazi zao za sanaa, au kama wazungu wanavyosema, Management.
Wenyewe, hasa chipukizi wanaotaka kutoka, utawasikia wanasema, nina kipaji lakini sina meneja. Ingawa wanaposema meneja maana yake ni msimamizi wa kazi zao, lakini kwao huwa na maana pana zaidi, kwamba mtu huyo, ndiye awe bosi wake, amsaidie hela ya studio, kazi ikitoka aipeleke redioni kisha awe ndiye msimamizi na mpangaji wa kila kitu chake.
Mikataba wanayoingia na mameneja hawa, huwaonyesha wao kama waajiriwa. Baada ya hapo ni kufuata amri zao, ndiyo maana unaona wasanii wanakejeliwa hadi kuwekwa mitandaoni eti wanawaomba misamaha mameneja wao. Inatisha!
Ukweli mmoja ambao wasanii wetu wanashindwa kuelewa ni kwamba wao ndiyo mabosi, wao ndiyo hasa wanapaswa kunyenyekewa. Meneja hawezi kuingiza hela kama msanii hapati shoo, hauzi kazi zake wala hapati matangazo. Kazi ya meneja ni kutafuta kazi, akishapata anarudi kwa bosi wake na kuweka mezani mazungumzo ya masilahi. Ni wajibu wa msanii kukubali au kukataa kutegemea na jinsi anavyojichukulia.
Lakini huku ni kinyume chake, meneja anazungumza kila kitu kuhusu kazi na masilahi, msanii wetu anaambiwa tu panda jukwaani, malipo yako haya hapa!Nimegundua kwa nini wasanii wetu wengi wanaendelea kuwa kama walivyo baada ya kuongea na mmoja kati ya mameneja wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayeitwa Babu Tale.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment