0
Kwa hili atachomoka?: Emmanuel Okwi mara kwa mara ameingia katika migogoro ya soka
Bado kuna ‘ giza ‘ katika usajili wa mshambulizi, Emmanuel Okwi kutoka timu ya Yanga SC na kujiunga na Simba SC, lakini nyuma yake tayari kuna baadhi ya malamiko ya msingi ambayo baadhi ya timu wamepeleka katika ‘ Kamati ya nidhamu ya TFF’ kwa sababu za kukiukwa kwa kanuni, sheria na taratibu za uhamisho wa wachezaji.

Kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, kiongozi mmoja wa klabu kubwa nchini alimfuata mchezaji, Salim Mbonde wa klabu ya Mtibwa Sugar na kumwambia ‘ tunataka kukusajili’. Mbonde mchezaji chipukizi wa Mtibwa alimjibu kiongozi huyo kuwa; ‘ Bado nina mkataba wa  miaka miwili na timu yangu’. Yalikuwa ni majibu ya hekima na busara kutoka kwa mchezaji huyo.
Siku zote ni makosa mchezaji kuzungumza mambo ya usajili na timu nyingine kabla ya klabu kufahamu kwanza. Mchezaji alitambua hilo lakini ajabu kiongozi huyo ambaye yupo pia katika kamati nne za Shirikisho la soka nchini, huku akihodhi pia nafasi ya ungozi wa juu katika klabu yake na chama cha soka ni wazi hakuwa akifahamu lolote kuhusiana na anachotakiwa kufany


Usajili wa Abdi Banda kutoka Coastal kwenda Simba una utata pia.
Licha ya kujibiwa hivyo, bado kiongozi huyo aliendelea kumshawishi mchezaji huyo na kumwambia ‘ Nenda kavunje mkataba kwa Jamal Bayser ( kiongozi wa Mtibwa Sugar) tutakuja kukusajili’. Je, unategemea nini kutoka kwa kiongozi wa namna hii hasa wakati ambao anatakiwa kuvaa uhusika wa nafasi yake kama mmoja wa wajumbe wa Kamati ya utendaji wa TFF?.

Ukiona wachezaji wanasajiliwa bila ya kufuatwa kwa taratibu tambua nyuma yake kuna nguvu ambayo huwafanya kukubali japo ni makosa ambayo yapo wazi katika kanuni za usajili.
Itakuwa ni kuendelea kupoteza imani endapo wachezaji kama Emmanuel Okwi, Abdi Banda, na Shaffih  Hassan wataruhusiwa kucheza mpira msimu ujao kutokana na makosa waliyofanya.
Okwi bado ana mkataba na Yanga kama ambavyo mwenyekiti wa klabu hiyo alivyowahi kusema, Banda bado ana mkataba wa miaka miwili na Coastal Union wakati Shaffih alisaini mkataba wa muda mrefu na klabu ya Ashanti United mwishoni mwa mwaka uliopita.

Wachezaji hawa wote watatu wana mikataba na klabu mbili kwa wakati mmoja. Ni wapi imewahi kufanyika jambo kama hilo? Ni Tanzania tu huku watu wanaofanya hivyo wakiwa ni viongozi wa juu wa mpira ngazi ya Taifa.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi na viongozi wa chini yake waachane na maamuzi ya busara badala yake wafuate sheria.
Kama kweli ipo nia ya dhati ya kukomesha vitendo hivyo, basi ni kuanza kuchukua hatua kwa viongozi wa klabu ambao wanakwenda kuwashashi wachezaji wa timu nyingine kuvunja mikataba na klabu zao hili tu wapate urahisi wa kuwapata wachezaji hao.
Mchezaji anaweza kucheza mahali kokote endapo hakutakuwa na tatizo linalomzuia, ndiyo maana klabu kubwa dunia zinafanya biashara ya kuuziana wachezaji badaa ya viongozi wa timu hizo kukutana na kukubaliana.
Real Madrid ni mfano bora, ni klabu kubwa na yenye mafanikio barani ulaya, tazama walichofanya msimu huu uliopita wa usajili. Ton Kroos alisajiliwa na timu hiyo kutoka klabu bingwa ya UJerumani Bayern Munich, wakati huo huo kiungo Xabi Alonso akitoka kwa mabingwa hao na kujiunga na Munich, si hao tu vipi kwa biashara yao na Manchester United? Imekwenda safi na mahusiano yao yanaendelea kukua tangu wakati ule wa kina David Beckham, CrIstiano Ronaldo na sasa kina Angel Di Maria na Javier Hernandez.
United pia imekuwa na mahusiano mazuri na klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno lakini uzuri huo hauji kwa kuvunjwa kanuni na sheria za usajili zaidi ya kuzilinda kwa manufaa ya mpira wa miguuu.
Okwi haishindikani kutoka Yanga lakini unaweza kujiuliza Yanga ni wajinga hadi wamng’ang’anie?. Je, Coastal wamekosea kumfungia Banda, ni maswali ambayo hayatakiwi kwa sababu kanuni zinavunjwa na watendaji wenyewe mambo haya yanakuwa yakiumiza uoande mmoja, mtendwa huumia, na hujipanga kutumia mbinu bora zaidi kulipiza kisasi wakati ujao.
Yanga waliwachapa bao Simba wakati walipomsainisha Mrisho Ngassa, Simba walilalamikia lakini wakaishia kulipwa fidia, huku mchezaji huyo akifungiwa michezo sita tu.
Yalikuwa makosa, lakini si wakati wa kuendelea kufanya mambo kwa kutumia ‘ historia mbaya ya matukio yaliyopita’. Ngassa alitakiwa kufungiwa mwaka mmoja kama inavyotakiwa kuwa kwa kina Banda, Okwi, na Shaffih hivi sasa lakini kama maamuzi ya busara yataendelea kutumiwa na kanuni kuwekwa kando, mwakani viongozi wa timu nyingine watafanya hivyo kwa sababu tayari wengine wanaruhusiwa.
 

Post a Comment

AddThis

 
Top