Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Makubwa! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amefungukia madai ya kutoka na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moze Iyobo ambaye ni mume wa mtu akisema hakuna ukweli wowote zaidi ya kutaka kuchafuliwa.Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Aunt ambaye gazeti la Risasi Mchanganyiko liliripoti tukio la kutaka kufanyiziwa na mke wa dansa huyo aitwaye Mwengi Ally, alisema anamshangaa mwanamke huyo lakini ili kumkomoa atahakikisha anafanya kweli ili kama ni kunuka, kinuke kihalali.
Alisema kwamba yeye ni mke wa mtu asiyeweza kujirahisi kwa kutembea na kijana huyo na kwamba kama ni kujuana ni kwa sababu ya Diamond ambaye ni shemeji yake kwa Wema.
“Amenichafulia sana, siwezi kutembea na Moze, najiheshimu. Lakini kwa kuwa ameamua kunipakazia, nitahakikisha namtega mumewe na nikimnasa nampa penzi ili kama ni hizo vurugu azifanye kihalali,” alisema Aunt na kusisitiza:
Dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moze Iyobo (kulia).
“Siwezi kuwa na uhusiano na Moze, yule mwanamke alikuwa na nia ya kuifanya jamii inifikirie vibaya lakini amenoa.”Hivi karibuni kundi la watu likiongozwa na Mwengi lilifika nyumbani kwa Wema Sepetu likimsaka Aunt ili kumshikisha adabu kutokana na madai ya kutoka na mume wa mtu huyo.
Post a Comment