0
Tanga. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani hapa, kimepata pigo baada ya makatibu wawili na wajumbe tisa wa kamati ya utendaji, kujiuzulu na kujiunga na Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Waliojivua nyadhifa hizo ni Katibu wa Wilaya ya Tanga, Khalid Rashid pamoja na Husna Mawe wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha). 

Wajumbe waliojiuzulu ni Hussein Baruti, Mohamed Kidege, Hassan Maulid, Juma Yunusi, Zaina Manyeki, Seleman Hassan, Mwanaisha Kambimbaya, Mohamed Sululu na Kisua Mrami Kisua ambaye pia ni mweka hazina. 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Rashid alidai kuwa sababu za kujitoa zimetokana na kuandikiwa barua ya kusimamishwa uongozi kinyume cha katiba huku akipewa tuhuma kumi zisizo na ukweli. 

Miongoni mwa tuhuma hizo ni kupingana na maelekezo ya kamati kuu kuhusu kumvua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe. Sababu nyingine ni namna uongozi taifa ulivyoshughulikia suala lake kishabiki bila kufuata taratibu.

Post a Comment

AddThis

 
Top