0
Gor Mahia ya Kenya ilijiweka kwenye mazingira magumu ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame, pale ilipokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri, mbele ya Atletico club ya Burundi, kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Nyamirambo.

Huu ni mchezo wa pili kupoteza kwa mabingwa wa zamani wa lililokuwa kombe la washindi barani Afrika, Gor Mahia, baada ya pia kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya KCCA ya Uganda kwa kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Matokeo haya yanaifanya timu hiyo inayoongozwa na Mskotland Bobb Williamson ambae atachukuwa kibarua cha kuifunza Harambee stars ya Kenya mara baada ya mashindano haya ya kombe la Kagame, kushika mkia kwenye kundi la B, ambapo timu zilizosalia za APR, KCCA, Atletico na Benadir, zikiwa na pointi tatu kila moja.
Matokeo ya mechi nyingine
Polisi Rwanda 3 Vitalo 1
Hii ilikuwa ni mechi kali mno kwa sababu ilikuwa na kasi kubwa sana mwanzo mwisho..


Huyo jamaa aliyesimama wa pili toka kushoto, alikuwa anacheza sentahalf kwenye ile timu ya Ivory Coast iliyokuwa na akina Kipre Tchetche ambayo ilialikwa kwenye Challenge iliyopigwa Dar na Kilimanjaro ikatwaa ubingwa ana mwaka wa 4 sasa na El Mereikh


Kikosi cha Atletico

Kikosi cha Gor Mahia




kikosi cha Polisi Rwanda.

Kikosi cha Vitalo

Post a Comment

AddThis

 
Top