TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kuondoka mkoani Tanga kesho kuelekea Visiwani Pemba kwa kutumia usafiri wa Ndege kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara itakayoanza Septemba 20 mwaka huu.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa timu hiyo itaondoka kesho saa tatu asubuhi kwenye uwanja wa Ndege jijini Tanga wakiwa na msafara wa wachezaji 28 na viongozi sita.
Assenga amesema kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kwenye viwanja vya Migombani visiwani humo asubuhi na jioni wakiwa na lengo kuu la kuhakikisha wanajiandaa vema na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Amesema kuwa kati benchi la ufundi litakuwa likiongozwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Yusuph Chippo, Msaidizi wake Benard Mwalala, Kocha wa Makipa Razack Siwa na daktari wa timu na mtunza vifaa.
Post a Comment