0

Ushabiki ni kitu cha kwanza katika mpira wa miguu. Shabiki ni mtu anayependa ‘ kupita kiasi’ kile anachokuwa anashabikia. Kama huna sehemu unayoshabia basi si rahisi kupata ‘ ladha halisi ya mpira waiguu’.
Kupitia timu nayoishabikia naweza kuona makosa ya kiufundi, kufurahia ushindi, na vilevile kupata maumivu makali. Leo hii, maisha ya furaha ya mashabiki wa Manchester United yapo katika mashaka, ile furaha ya kushangilia ushindi kila mwisho wa wiki si ya kuaminika tena.
 
Lakini ni hapo shabiki anaweza kuona mapungufu ya timu yake, na pengine akajiaminisha kuwa ‘ usajili zaidi hauepukiki’. 

Kila mtu anaona udhaifu wa United hivi sasa. Baada ya kipigo katika uwanja wa Old Trafford kutoka kwa Swansea City siku ya ufunguzi, United ilisafiri hadi Kaskazini Magharibi mwa England na kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Sunderland katika uwanja wa Stadium of Right. United imefanikiwa kumsaini kiungo mshambulizi wa kimataifa wa Argentina, Angl Di Maria kutoka Real Madrid kwa ada ya rekodi England, pauni million 60. Di mAria amevunja rekodi ya usajili iliyowekwa na Fernando Torres Januari mwaka 2011 alipojiunga na Chelsea kwa ada ya pauni million 50 kutoka Liverpool.

Kabla ya msimu wa ligi kuu England kuanza, United ilikuwa katika kipindi kizuri cha maandalizi nchini Marekani. Huko waliweza kupata ushindi dhidi ya timu za AS Roma, Inter Milan, Real Madrid, Liverpool, kabla ya kuishinda, Valencia siku chache kabla ya kuanza kwa msimu. Timu ilionekana bora chini ya kocha mpya, Luis Van Gaal. Wachezaji wa safu ya ulinzi, Criss Smalling, John Evance, na Phill Jones walionekana kuimarika na kucheza vizuri katika mfumo wa 3-5-2 ambao unawapa uhuru wa kushambulia na kukabia katikati ya uwanja walinzi wa pembeni. 

Van Gaal ametokea kuwaamini sana wachezaji hao wa Kiingereza, lakini baada ya kushuhudia safu yake ya ulinzi ikiruhusu mabao mawili katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Swansea, Van Gaal aliharakisha usajili wa mlinzi wa kushoto wa Argentina, Marcos Rojo kutoka klabu ya Sporting Lisbon. Rojo ana uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi wa kati lakini wakati huu Luke Shaw akiwa katika majeraha, Van Gaal alimuhitaji, Rojo kucheza nafasi ya beki wa kushoto ambayo kiungo, Ashley Young alicheza katika mchezo wa kwanza. Smalling aliumia katika mchezo dhidi ya Sunderland, na walinzi wengine si wa kuaminiwa moja kwa moja kwa sababu, Jones na Evance wote ni wachezaji wa ‘ wasiwasi’ ni wachezaji wazuri lakini muda wowote wanaumia. 

Kuondoka kwa manahodha wote wanne kwa mpigo ni tatizo lakini tatizo zaidi ni kuwa wachezaji watatu walikuwa sehemu ya ulinzi. Patrice Evra, Rio Ferdinand na Nemanja Vidic hawa walikuwa msingi wa timu katika ngome. Van Gaal hatajuta kuondoka kwa wakongwe hao, lakini mashabiki wataendelea kuona mapengo yao katika ngome ya United kama hataingia sokoni kuongeza walau mlinzi mmoja wa kati. Safu hiyo imekosa kiongozi sahihi, majukumu ambayo yalikuwa yakifanywa na Rio, Evra na Vidic.

Usajili wa Di Maria umekuja wakati mwafaka. United hushambulia na kumaliza mechi kupitia pembeni ya uwanja. Huo ndiyo utamaduni wa kiuchezaji katika timu hiyo na Sir Alex Ferguson alifanikiwa kwa sababu hiyo. 

Van Gaal atapata shinda katika mfumo aliokuja nao, lakini ujio wa Di Maria unaweza kumsaidia kwa sababu tayari ana uhakika wa kuwa na winga wa hatari ambaye anauwezo wa kukimbia na mpira ama bila mpira katika eneo la pembeni ya uwanja. United ina uhakika wa kufunga mabao, lakini safu ya ulinzi haina uwezo mkubwa wa kulinda lango lao. 

Van Gaal ametumia pauni millioni 60 kumsaini, Di Maria, pauni millioni 16 kwa Rojo, na pauni millioni 17 kwa Shaw, wote hao hawajatia mguu uwanjani hivyo kuna uwezekano mkubwa wakainyanyua timu hiyo kuanzia wikendi ijayo, ila usajili wa nyongeza katika ngome utasaidia kuziba nyufa za wachezaji wanaokumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Usajili wa bei mbaya wote ulichemsha England, Juan Sebastian Veron, Robinho, Fernando Torres, ila sitaraji hivyo kwa Di Maria.

Post a Comment

AddThis

 
Top