WINGA wa Bayern Munich, Arjen Robben ameweka wazi kuwa bado hajawa fiti kucheza akitokea katika mapumziko, baada ya kumaliza kucheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil akiwa na timu ya taifa ya Uholanzi.
Mholanzi huyo alikuwa miongoni mwa nyota wa Louis van Gaal waliofika hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo na kutolewa kwa mikwaju ya penalty na Argentina.
Robben mwenye miaka 30 aliikosa mechi ya DFL-Supercup dhidi ya Borussia Dortmund na anahisi anahitaji kujifua zaidi ili kujiimarisha na kuanza kuiwakilisha Bayern.
“Ndivyo tulivyokubaliana kwasababu mechi ilikuwa karibu sana,” aliiambia tovuti rasmi ya klabu alipoulizwa kutokuwepo katika mechi hiyo.
“Nahitaji kufanya mazoezi ya nguvu kwa siku chache na kurudisha kasi yangu. Bado nipo katika maandalizi ya kabla ya msimu. Hamu ya kucheza mpira bado haijaja. Nipo tayari kuanza upya”.
Post a Comment