0


Mmiliki na mwenyekiti wa timu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo Moise Katumbi amesema ana mpango wa kuiimairisha timu hiyo ili iwe na nguvu ya kushiriki katika mashindano ya kidunia, Katumbi anaamini kuwa anaweza kuifikisha timu hiyo katika ngazi ya fainali za kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu.

Pamoja na TP Mazembe kushindwa katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF lakini bado Katumbi anasema anajiandaa vyema na msimu ujao na mashindano mengine."Malengo yetu ni kuleta ushindani mkubwa na ninaamini tunaweza kufikia mafanikio kwa kile tulichonacho sasa"alisema Katumbi.

Katumbi pia ameiambia BBC kuwa iwapo wataimarisha zaidi timu yao na kwamba haoni ni kwanini siku moja TP Mazembe siku moja wasishinde kombe la dunia.

Mwaka 2010, timu hiyo ya soka ya Mazembe ndio iliyokuwa klabu ya kwanza toka bara la Afrika kutinga fainali katika mashindano ya kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu lakini wakaondolewa na klabu ya Inter Millan ya Italia.

Baada ya michuano hiyo ya michuano hiyo ya shirikisho timu hiyo toka mji wa Lubumbashi nchini Demokrasia ya Congo wanatarajiwa kurejea tena katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka ujao.

Tambo hizi za Mazembe ni kutokana na vipaji vya kutosha kutoka katika shule ya vipaji vya michezo ambapo wanatarajia baada ya miaka mitatu wantakuwa na wachezaji wenye uwezo wa kuwafikisha na kushinda kombe la dunia.

Hata hivyo Katumbi kiongozi wa miongoni mwa timu tajiri barani Afrika amesema kuwa ameweza kuhakikisha fedha zinapatikana ili kuimarisha kikosi chake,kutengezeza uwanja mpya na wa kisasa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege ya timu.
Mipango yake katika kupata wachezaji wa kimataifa inaendelea ambapo kwa sasa anawachezaji nchi za nje ambapo kwa ana wachezaji kutoka nchi za Tanzania, Ghana, Zambia, Cameroon, Botswana na hivi karibuni amesajili kutoka Malawi.

Timu hii ya TP Mazembe ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wake wanalipwa vizuri kwa viwango vya Afrika ikiwa ni jitihada za Katumbi kupunguza kaksi ya vipaji vya Afrika kupotelea ulaya.

"Wachezaji wazuri wa Afrika wanakwenda ulaya kwa sababu ya malipo mazuri kutokana na kutolipwa vizuri hapa Afrika" anasema Katumbi.

Katumbi anasema kuwa sera yao ni kuwachukua wachezaji toka nchi za Afrika ili kuonyesha umoja ndania ya bara hilo na kwamba Afrika ni nnzuri lakini kinachotakiwa ni umoja hasa kutokana na mapigano ambayo yamekuwa yakitokea kila siku katika bara la Afrika.



Post a Comment

AddThis

 
Top