0
Usajili wa wachezaji kwa dirisha dogo kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara unafunguliwa Novemba 15 mwaka huu na utafungwa rasmi Desemba 15 mwaka huu.

Kwa mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.

Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date.

Matukio mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Nairobi, Kenya.
Juma Kaseja akisaini mkataba wa kuichezea Yanga mbele ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Bin Kleb, nyuma Abdulfatah. Kaseja amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.

kaseja na kleb wakihakiki jinsi mikataba ilivyosainiwa 



Post a Comment

AddThis

 
Top