Mzigo wa kilo 300
Hakuna jambo lisilowezekana - labda hayo ni mawazo yangu lakini ukiangalia pich na jinsi mzigo ulivyo utaona kabisa kuwa kukosa gari sio mwisho wa kubeba kilo mia 300 kwenye baiskel,hapo hakuna tena kuendesha,ni kuisukuma baiskeli. Amefunga kamba kwenye usukani ili aweze kuiongoza baiskeli yake vizuri
kama unavoona mizigo inabebwa kama kawaida
Mara nyingi watu wanahitaji muda wa masaa mengi kwenda shuleni au kwenda kuchota maji, kutafuta kuni au chakula. Katika maeneo mengi hakuna usafiri wa umma, magari yanauzwa kwa bei kubwa sana. Hivyo wakati mwingine watu wanashindwa kusafirisha bidhaa zao. Lakini mkulima huyu amepata suluhisho. Anaweza kupeleka bidhaa zake sokoni kwa kutumia baiskeli.
hapa kuku wanafika sokoni bila tatizo
Usukani wa baiskeli unaweza kubeba kuku wangapi?Wakati mwingine anauza baadhi ya kuku wake njiani. Lakini nia yake ni kuwapeleka sokoni ambapo watu huuza bidhaa freshi. Ndiyo maana kuku hawa hawajachinjwa.
Mee, mee
Mbuzi hawa wamebananishwa kweli! Mmiliki wao anawapeleka mnadani. Bei ya mbuzi ni makubaliano
Huyu baba hana familia yake hana gari lakini kama kawaida wanakwenda wanapopataka na wanafika bila tatizo
Mambo ya kukata kiu na vinywaji laini kama soda hizo zinapelekwa dukani
Mtu anayemiliki duka bila kuwa na gari la kusafirishia mizigo lazima atafute mbinu ya kubeba bidhaa mpya kwa ajili ya duka lake. Nchini Tanzaniabidhaa hizo hutolewa mijini na kupelekwa sehemu za ndani kabisa vijijini.
KWA STYLE HII BAISKELI NI USAFIRI TOSHA
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.