0
RPC  Ramadhan Mungi.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wamekamatwa  na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa  na  kuhojiwa  kwa  masaa  matatu.
Viongozi hao   walikamatwa  majira ya saa 3 asubuhi katikati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge.

 Akithibitisha kukamatwa kwa  viongozi hao ,  kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa viongozi hao walikamatwa kwa mahojiano kutokana na kutoa kauli hatarishi kwa amani ya  Tanzania wakati wa mkutano wao uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kwa ajili ya mabaraza ya ukusanyaji wa maoni ni rasmu ya katiba.

Kamanda Mungi amesema kuwa kibali ambacho Chadema walipewa kilikuwa kikianza saa 9 Alasili hadi saa 12 :00 ila wao waliendelea na mkutano huo hadi majira ya saa 12 .25 na kila walipofuatwa zaidi ya mara moja kuelezwa kuhusu muda wa kibali chao kuisha bado viongozi hao waliendelea kuendesha mkutano huo huku wakitumia vipasa sauti kutoa maneno ya dhahaka dhidi ya jeshi la polisi. READ MORE

Post a Comment

AddThis

 
Top