0
STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amewavaa baadhi ya watu wanaoponda kitendo cha yeye kukubali kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwa maelezo kuwa ni kama maigizo kwani ndoa hakuna
Staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akionyesha pete aliyovishwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Shilole alisema anawashangaa wanaodhani ataishia kuitwa mchumba tu bila kuiona ndoa, akasema anachojua ndoa itafungwa siku si nyingi kwani wanapenda kwa dhati
“Kama ilishindikana kwao ni kwao tu, sisi ni watu wazima tunaojielewa na mpaka hapa tulipofikia hakuna kitakachoharibika. Tunapendana hivyo panapo uzima Mungu akijaalia ndoa itafungwa,” alisema Shilole.

Post a Comment

AddThis

 
Top