TUMKUMBUKE » PEPE KALLE » KABASELE MIAKA 16 TOKEA AFARIKI DUNIA
Nakumbuka Ilikua Siku ya Jumamosi Tarehe 28 November 1998, pale niliposikia Habari ya Kusikitisha Kuhusiana na Kifo cha JEAN – BAPTISTE KABASELE – YAMPANIA Maarufu kwa Jina la » PEPE KALLE « . Kafa kutokana na Mushtuko wa Moyo kwenye Hospitali ( KLINIKI ya NGALIEMA ) JIJINI KINSHASA.
Bonge la Mtu huyo kaondoka, Alikua Mrefu wa kimo unao karibia Mita 2,10 na Uzito wa takriban Kilo 150. Ndie huyo Kiongozi wa Orchestra » EMPIRE BAKUBA » Akishirikiana na Wenzie » PAPY TEX « , na » DILU DILUMONA » , SESKAIN MOLENGA…
PEPE KALE ni mmoja kati ya Wanamuziki walio wengi Inchini CONGO ambao wamejifunza kuimba kutokana na Mchango Mkubwa wa Kwaya la Kanisa Katoliki.
PEPE KALE katokea kuupenda Sana Muziki, ndoto yake kuu ilikua azifwate nyao za kipenzi chake kwenye Fani hiyo, si mwengine bali ni Star kuwazidi wengine wote kwa wakati ule » JOSEPH KABASELLE » ( KALLE JEFF ). Ndie aliekua kama Mdhamini na Fundi wake kwenye Kazi ya Muziki.
Kadri siku zilivyozidi kuendelea, Kijana » PEPE KALE » kaonyesha dalili zakutaka kujitegemea, ajijengee mwenyewe aina yake ya Uimbaji na baadae kuunda Group lake.
KABASELE YAMPANIA » PEPE KALE « , kazaliwa JIJINI KINSHASA Tarehe 30 -12- 1951. Wazazi wake ni wenyeji wa Mkoa wa » KASAÏ YA MAGHARIBI » katikati mwa Inchi ya CONGO.
Kwenye Miaka ya 1968- 1969, Kabla bado hajawa Maarufu sana, » PEPE KALE » kapitia kwenye Group kadhaa za Muziki JIJINI KINSHASA, Tutazitaja ( Group ZULU, AFRICA CHOC, MYOSOTIS … ). Na baadae kaja kujiunga na Orchestra » BELA – BELA » chini ya umiliki wa Ndugu » SOKI VANGU na SOKI DIANZENZA « , pamoja na Ushirikiano wa mwimbaji Mahiri » NYBOMA » .
Katika Kipindi hicho » PEPE KALE » akiwa bado hajawa maarufu, hajafaanikiwa kurekodi Nyimbo nyingi, kati ya chache alizoziweka, tutazitaja : ( NAZOKI, NA KO BELELA, LIBAKU …) .
Orchestra EMPIRE BAKUBA, ikilinganishwa na nyingine, hutokea kua Imara zaidi, mara chache sana kuwaona Wanamuziki wakijiondoa kwenye Group hilo. Katika kipindi cha Miaka 26, Orchestra EMPIRE BAKUBA lilitamba kweli kwenye Pembe zote za Dunia, Nakutoa SHOO kali zilizo sisimua Mashabiki na Wapenzi wa Muziki kwa jumla.
Kutokana na Ujuzi wake wa Kazi, » PEPE KALE » kapewa Tuzo nyingi za Kimataifa, Kati ya tuzo hizo, lililo la kifahari zaidi ni Tuzo kapewa na ( RADIO FRANCE INTERNATIONAL ) Mwaka 1991 kama Msanii Mwanamuziki Bora » AFRO – CARIBEAN » .
Kadhalika » PEPE KALLE » na Orchestra » EMPIRE BAKUBA » wamepewa kwa mara Kadhaa Tuzo nyingi pia za Kitaifa, zikiwemo : ( MSANII BORA, MTUNZI BORA WA NYIMBO , ORCHESTRA BORA …).
Group » EMPIRE BAKUBA « , walikua Wabunifu wazuri wa Dansi, Wakiwashirikisha Madansa wao Mashuhuri akina » EMORO ambae kafariki Mwaka 1991, JOLI BÉBÉ, DOKOLOS, DOMINIQUE MABWA, Bila kumsahau BILEKUMPASI « , Pindi wapandapo Jukwaani watachangamsha hadi mwisho wa SHOO.
Kadhalika, Watakumbukwa kwa ubunifu wa Miondoko ya Dansi, kutokana na Mchango Mkubwa wa Orchestra » EMPIRE BAKUBA » Dansi kadhaa zilifahamika zaidi. Tutazitaja : ( MASASI CALCULER, SOUS MARIN Ô NAGER, KWASA – KWASA …) .
Katika Uhai wake, PEPE KALLE alikua Mtu asiependa matatizo na wengine, Alikua mpole na Mwema sana, Wengi hukubaliana kwa Sifa hizo. Kaacha hisia nzuri kabisa dhidi yake.Kifo chake cha ghafla Miaka 16 iliopita, kilileta Udhuni na Majonzi kwenye Familia yake, na kuacha Pengu kubwa kwenye Muziki wa CONGO.
Utakumbukwa Daima
Post a Comment