Bunge la jumuiya ya Afrika mashariki huenda likafungwa iwapo baadhi ya viongozi wakuu wa Afrika mashariki hawataingilia kati kufuatia migogoro ya takriban miezi sita sasa inayolikumba.
Hali hiyo inatokana na kwamba mataifa yaliowachagua viongozi hao kama wawakilishi wake hayana uwezo wa kuwaadhibu wabunge hao.
Bunge la Tanzania limekiri kwamba halina uwezo wa kuwasimamisha kazi wawakilishi wake katika bunge hilo, licha ya kwamba wanaendelea kuzozana.
Hatua hiyo inajiri baada ya chama cha FDC nchini Uganda kulitaka bunge la nchi hiyo kuwafuta kazi wawakilishi wake kwa kuwa wabunge hao hawatekelezi wajibu waoBendera za maitaifa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Bunge la EALA limeshindwa kufanya kazi katika miezi iliopita huku wanachama wakiwa na mpango wa kumuondoa Spika wa bunge hilo Maregeret Zziwa kwa madai kwamba ameshindwa kutekeleza wajibu wake inavyohitajika.
(CHANZO: BBC SWAHILI
Post a Comment