0



MZEE PAPA WEMBA ndie aliekua Mualikwa kwenye Kipindi cha  » BAKOLO MINDULE « . kasema yeye ndie Mwalimu Mkuu wa Muziki CONGO, na Group lake VIVA LA MUSICA ndo chuo walipopitia wengi mnao wafahamu.
Kawatambulisha Kinadada waimbaji wa 5 ambao wameingia Chuoni ilikujihimarisha zaidi kwenye Muziki.  Wamejitambulisha kama ifwatavyo :
1. MARIA LIKONZI ( Katokea kwenye Chuo Kikuu cha Muziki Jijini KINSHASA ( INAS ) Kasema amefaidi sana kuakwake pembeni ya PAPA WEMBA.
2. JOLIE THISHIMBI MULUBA ( Katokea pia Chuo Kikuu cha ( INAS )
3. DORAH ni Mdogo yake MARIA LIKONZI
4. CHRISTELLE VOMANKOY
5. BENEDICT LA DIVA, yeye kaanza kama Mnenguaji,hadi leo hii  kawa Mwimbaji. Miaka 12 sasa yuko kwenye Group VIVA LA MUSICA.
PAPA WEMBA kasema  » J’aime la femme  » / NAMPENDA SANA MWANAMKE,  SEHEMU WALIPO AKINA MAMA HUA HAPAKOSI AMANI. anayo furaha kubwa kufanya kazi na Wanawake, Sauti zao zinahitajika kwenye Muziki wa CONGO. kama wanavyo jitetea vizuri Dada zetu akina TSHALA MWANA, MJ 30, MBILIA BEL…
PAPA WEMBA anaendelea kusema kwamba, Mwanamke ndie Msingi wa Jamii wa Inchi, Sote hutokana kwanza na Mwanamke, Ndie Mzazi wa kwanza, ndie mlezi namba 1. Ila kwa Siku hizi Baadhi ya Akina Mama wengine Hupotosha maadili ya Umma kutokana na mwenendo wao mbaya, Uvaaji wa mavazi nusu Uchi.
Kasema, Ugonjwa wa Ebola, haupo tena CONGO, kwa wale ambao wanaendelea kuathirika nao, wanakaribishwa Inchini CONGO ili wapewe Mbinu ya kupambana vilivyo na maradhi hayo.

Post a Comment

AddThis

 
Top