0
Stori: Gabriel Ng’osha

Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki, anayefananishwa na aliyekuwa staa wa Bongo Fleva, marehemu Alberth Mangweha ‘Ngwea’, ameingia katika mzozo mkali na ndugu zake akidaiwa kugombea maiti ya mama yake mzazi, Mariamu Enock (54).

 Kijana Mohamed Said almaarufu Ngwea feki.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri kwenye makazi ya familia hiyo, Tandale, Dar hivi karibuni ambapo mama huyo alifariki dunia kwa kuugua kwa muda…
    ngwea feki akizozana eneo la msiba
Ilidaiwa kwamba, baada ya kifo hicho, uliibuka mzozo ambapo ndugu wa upande wa mama yake walitaka mwili wakaupumzishe mkoani Iringa huku Ngwea feki akitaka uzikwe Dar. Ilisemekana kwamba jamaa huyo alitaka iwe hivyo kwa sababu alikuwa na mama yake muda wote na alitumia gharama kubwa kumtibu.
       kaka wa ngwea feki hassan said

 Akizungumza na mwanahabari wetu kuhusiana na sakata hilo, msemaji wa familia hiyo, Laurence Enock ambaye ni kaka wa marehemu (yaani mjomba wa Ngwea feki), alisema:  “Sisi kama familia tumeamua kumsafirisha ndugu yetu kwenda kumzika Iringa, ndiko kuna mashamba ya familia yetu lakini Mohamed (Ngwea feki) amekataa.”
           baba wa marehemu babu yake ngwea feki mzee enock mayenje

Alisema kwamba, baada ya vuta nikuvute ndipo Ngwea feki akadai alipwe shilingi laki tatu (300,000/=) alizotumia kumtibu mama yake wakati anaumwa.Kwa upande wake, ndugu wa Ngwea feki aliyefahamika kwa jina la Hassan Said alionekana kutomuunga mkono ndugu yake.
                  ndugu wa ngwea feki hassan saidi kushoto akiwa eneo la tukio
Hassan alisema: “Mimi siko tayari kugawana vitu vya mama yangu kwa kuwa ndugu yangu amekataa mwili wa mama usisafirishwe hadi alipwe fidia yake hivyo imebidi tuuze vitu vya mama ili alipwe hiyo laki tatu.
wa pili kushoto ni msemaji wa familia hiyo lawrance enock kaka wa marehemu mjomba wa ngwea feki


Alipofuatwa Ngwea feki ili kusikia upande wake aligoma kutoa ushirikiano: “Siko vizuri kwa sasa nicheki baadaye.”
Kwa mujibu wa baba wa marehemu, Enock Mayenje, mjukuu wake huyo amekuwa akijitenga na familia hivyo hawezi kumlazimisha ila amesikitika kwa kitendo chake cha ‘kuwauzia’ maiti ya mama yake mzazi.

              marehemu mariam enock enzi za uhai wake
Kamanda wa Ulinzi Mtaa wa Mkunduge, Tandale jijini Dar, Yusuph Banda, amekiri kutokea kwa tukio hilo na wamekubaliana kuuzwa kwa vitu vya marehemu ili gharama hizo zilipwe kwa Ngwea feki ili mwili huo usafirishwe kwenda Iringa kwa mazishi.Kujua mengi zaidi kuhusu tukio hilo, tembelea www.globaltv.tz

Post a Comment

AddThis

 
Top