0



Mawasiliano kati ya Marehemu BABIA NDONGA CHOKORO na JB MPIANA yalikua mazuri kabisa, Wakati BABIA NDONGA akimlalamikia Boss wake wa zamani KOFFI OLOMIDE kumkataza athithubutu kufanya SHOO nakutumia Jina lake, JB MPIANA yeye kamruhusu Bila kusita.

Kupitia SHOO kadha alizofaanikiwa kuzifanya wakati wa Uhai wake akiwa Inchini ANGOLA, BABIA NDONGA kazirudilia Nyimbo kadhaa za JB MPIANA, ( OMBA, SANS TE TOUCHER…).

Kupitia Video tunayo ambatanisha na Post hii, SEGUIN MIGNON MANYATA ambae ndie Kiongozi wa Wanamuziki wa Group WENGE MUSICA BCBG, kayajibu Maswali kadhaa wakati akihojiwa na Mtangazaji MAMI ILELA.

SEGUIN MIGNON MANYATA kayanena haya : 1. JB MPIANA na Marehemu BABIA NDONGA walikua na uhusiano Mzuri na mwema, Salamu zetu za Rambi rambi ziwaendee Familia yake,

2. Group BCBG Hatujajitokeza pale Msibani, ila tupo Pamoja na Familia ya BABIA NDONGA, Hatupendelei tena hizo Tabia za Kujionyesha, Tabia za Umimi ndie kafanya hivi hatuzitaki kabisa. Ila Kwanjia moja au nyingine Tunaungana na Familia ya Marehemu.

3. Kutokana na Tamko kali la MEJA GENERALI CELESTIN KANYAMA, tunazitupilia mbali Tabia ya Malumbano, Kilicho chamuhimu nikuona kwamba Mazishi ilifanyika katika mazingira mazuri tena kwa usalama, Kama JB MPIANA PAPA CHERI hajajitokeza ilikua hasa kuhofia isije ikachafuka hali ya Usalama wa Raia. Mara nyingi Wakati Ma Leaders wa Muziki wanapo kutana hua panajitokeza hali ya Vurugu.

4.Kumbukeni Wakati wa Msiba wa Dansa Wetu  » Marehemu MONICA « , Palitokea na Kizazaa hadi kuna Mtu alie katwa Mguu wake, hadi leo hii JB MPIANA kashindwa kabisa kulisahau tukio hilo.

5. Mtu anapo fariki, kaondoka na alivyokua navyo moyoni mwake, Ila Watoto wake Bado wapo, siku zijazo, PAPA CHERI JB MPIANA ataenda kuwajulia hali ni ndicho kilicho cha muhimu kwa sasa.

Hata kama JB MPIANA hajajitokeza binafsi kwenye msiba, ila Mawazo yake ipo kwa watoto wa marehemu.

6. Wajua, Ingawa Mwenyezi Mungu angetenda miujiza kumuamsha BABIA NDONGA hata sekunde cheche, Wengi waliokua hapo Msibani wange chapwa fimbo. Hamna shida yeyote, MUNGU auweke Moyo wake mahala pema . SISI TUNAJUA NAMNA GANI TUTAKAVYO WAJALI WANAE.

Post a Comment

AddThis

 
Top