0
Mike Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni Seneta wa jiji la Nairobi.
Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta alikwenda The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya wenzake wanaopinga huo uamuzi wa ICC na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli zao ili kwenda kumsupport ambapo Seneta huyu ni mmoja wa waliojilipia na kulipia wengine pia.
Pamoja na Sonko kwenda huko akiwa na dukuduku la kukerwa na maamuzi ya Mahakama hiyo akiitaka imuache Rais wao wa Kenya afanye kazi, aliamua kuvaa tshirt yenye maandishi ya Kiswahili ‘ikiwatusi’ Wazungu kama anavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.

Post a Comment

AddThis

 
Top