TUMKUMBUKE DOKTA NICO KASSANDA ” BABA WAWAPIGA SOLO GITA “
NICO KASANDA WA MIKALAYI Aka DOKTA NICO, kazaliwa Tarehe 07-07-1939 Mjini LULUABOURG leo hii hujulikana kwa jina la KANANGA.
Kafariki Dunia JIJINI BRUSSELS Tarehe 22-09-1985 kwenye Hospitali ya SAINT LUC. Baada ya kuugua kwa Mda mrefu.
DOCKTA NICO KASANDA katokea kwenye Familia ya Wasanii, Baba yake Mzazi akiwa ” accordionist “, Huku Kaka yake Mkubwa anaefahamika kwa jina la ” CHARLES MWAMBA DECHAUD ” akiwa Mpiga GITA mashuhuri.
DOKTA NICO KASANDA kajifunza GITA kutoka kwa Binamu yake ” EMMANUEL TSHILUMBA WA BALOJI Aka TINO BAROZA ” Mmoja wawapiga GITA Mahiri sana kwenye Historia INCHINI CONGO.
DOKTA NICO KASANDA,Msanii ambae ni Mkali kwa GITA kawa kishawishi kikubwa kwakizazi kizima cha Wapiga GITA Inchini CONGO,Tutawataja : GUVANO, ATHEL, DIZZY MANDJEKU, MAVATIKU, PEPE FELLY MANUAKU, ROXY TSHIMPAKA…
Tukiachia Mbali Inchi ya CONGO, Ushawishiwake kwenye GITA Umevuka mipaka hadi kwenye Baadhi za Inchi za Africa wanamkubali, kama alivyodai Mpiga GITA kutoka Inchi ya GUINEA ” SEKOU BEMBEYA ” kasema yeye ni mfwasi kamili wa DOKTA NICO KASANDA.
DR NICO KASANDA kakumbatia Fani ya Muziki akiwa bado Mdogo wa Umri wa miaka 14, Kaka yake DECHAUD ndo kamleta kwenye Group ” AFRICAN JAZZ ” nakumuunganisha na NYOTA wa Muziki wa Congo ambae si Mwengine bali ni ” JOSEPH KABASELE GRAND KALLE “.
Kabla yakuchagua kazi ya Muziki, DOKTA NICO KASANDA alikua Fundi mekanica JIJINI KINSHASA kwenye Kiwanda kinachotengeneza Mafuta yakupikia. na wakati alipoamua kujiunga rasmi na Muziki, kaanza kwenye sekta ya Uimbaji, Basi ikaja kutokea siku Moja Binamu yake ambae ndie Fundi wake Mkuu wa Gita ” TINO BAROZA ” hajatokea mazoezini, Kwakua DOKTA NICO
KASANDA tayari kesha jifunza Gita, Kapewa fursa yakushirikiana na Kaka yake ” DECHAUD “wakati wakiwa kwenye STUDIO ” OPIKA ” Kwenye matayarisho ya Wimbo Maarufu ” PARAFIFI ” Utunzi wake ” JOSEPH KABASELE GRAND KALLE . ” Studio ” OPIKA ” ilikua ikimilikiwa na ” MOUSSA BENATHAR “,
Ndipo kazaliwa Lengend NICO KASANDA. Wapenzi wake humpachika Jina la “mungu wa Gita ” . Kalisakata Gita pasipokua na Mpinzani…
Mwaka 1961, Tofauti ilijitokeza kati ya DOKTA NICO KASANDA na JOSEPH KABASELE LE GRAND KALLE , Kutokuwepo kwa maelewano katiyao, kukapelekea DOKTA NICO KASANDA kuchukua uamuzi wakujiondoa kwenye Group ” AFRICAN JAZZ ” na kaunda Group lake kalipa jina ” AFRICAN JAZZ aile NICO KASANDA “,
Akiwa Kwenye Group lake, Ndipo kamleta ROCHEREAU TABU LEY ambae alikua Mkalimani kwenye Shule ya ” ATHÉNÉE DE KALINA ” kwaleo hii hujulikana kama ” ATHÉNÉE DE LA GOMBE ” . Wakawa wanafanya mazoezi kwenye MTAA WA KIGOMA Manispaa ya KINSHASA .
Baadhi ya Nyimbo nzuri Mfano ” CHERIE STAROFINA ” , ” AFRICAN JAZZ MOKILI MOBIMBA ” walikua tayari wakizicheza mazoezini. Kwaupande wake JOSEPH KABASELE LE GRAND KALLE bado kaendelea kuwatumia kwenye GITA ” TINO BAROZA na EDO CLARY LUTULA ” .
Mwaka 1962, Baada yakuuwawa Waziri Mkuu na Shujaa wa Uhuru wa CONGO ” PATRICE LUMUMBA “, Baadhi ya Wabunge kutoka Mkoa wa ” STANLAYVILLE ” kwaleo ” KISANGANI “, Tutawataja akina : ( Waheshimiwa KIDISHIO, MBARIKO, BADJOKO ), waliingilia kati ilimzozo kati ya KABASELE JOSEPH GRAND KALLE na DR NICO KASANDA upate kupatiwa suluhisho. Kwa bahati nzuri muafaka ukapatikana , na wakaja kujiunga pamoja kwa mara nyingine tena. Wakafaanikiwa kusafiri JIJINI BRUSSELS kumalizia baadhi ya Nyimbo kwenye Studio za huko.
Mwaka 1963, Tofauti ya mapato ya Pesa ikajakujitokeza, Kwasafari hii DR NICO KASANDA kajiondoa kabisa nakwenda kuunda ” ORCHESTRA FIESTA ” akiwa pamoja na ROCHEREAU TABU LEY, ROGER IZEIDI, DECHAUD na MUJOS, Huku JOSEPH KABASELE LE GRAND KALLE akiendelea kusapotiwa na Mpiga Gita Hodari TSHILUMBA WA BALOJI Aka ” TINO BAROZA “
Tarehe 16-11-1965, GROUP AFRICAN FIESTA ikasambaratika, ROCHEREAU TABU LEY akaunda Group lake ” AFRICAN FIESTA NATIONAL, huku DR NICO KASANDA akawa Mmiliki wa ” AFRICAN FIESTA SUKISA
Mwaka 1966, DR NICO KASANDA kafaanikiwa kumiliki ” Musical Editions SUKISA ” pia kajitahidi kuliunda kwa upya Group lake ” AFRICAN FIESTA INTERNATIONAL “. Group hili lilikua Juu na kupeta sifa nyingi kwenye Muziki hadi pale ulipofikia Mwaka 1974.
Kwahapa yahitajika vizingatiwe vitu 4 Muhimu :
1. Timu ya waimbaji ilikua ikiongozwa na : APOTRE, VIGNY, MICKY, na MIZELE ,
2. Wanamuziki CHANTAL KAZADI ,na KUTU KABENGELE SANGANA wakaja kujiunga na Group Mwaka 1967. Kujiunga kwao kukapelekea watupwe benchi hao walio tangulia. kwakweli walileta Moto mkali wa aina yake kwenye Group, hasapale walipo onyesha umahiri wao wakuimba kwenye Nyimbo : ” Mbandaka “, ” Yaka Toyambana “, ” La Jolie Bébé “, ” Chantal “, ” Bougie ya motema “, ” Limbisa ngai “, ” Tu m’as déçu “, ” Marie Nella “, ” Je m’en fous “,” Saouda “…
3. Mwaka 1969, CHANTAL KAZADI na SANGANA wakajiondoa nakwenda kuunda Group lao ” AFRICA SOUL “
Ndipo pale walipoletwa kwenye Group AFRICAN FIESTA SUKISA Waimbaji ” LESSA LASSAN ” na ” KIAMBUKUTA JOSKY “, ambae kaja kuonyesha Umahiri wake wauimbaji kwenye Wimbo ” BOLINGO EZALI MPE NA KISI ” , na ulipo fikia Mwaka 1970 kaimba ” BOLINGO YA SENS UNIQUE ” kachaguliwa kama Mwimbaji Kinara wa Group hilo.
Mwaka 1972, KIAMBUKUTA JOSKY kajiondoa kwenye Group AFRICAN FIESTA INTERNATIONAL nakwenda kujiunga na Group ” CONTINENTAL “. kamuacha Dr NICO KASANDA katika Shida sana yakimpangilio kadhalika pia kipesa.
4. NICO KASANDA kajikuta yuko hoi, akiwa kwenye hali ngumu sana kimaisha, Ingawa kaja kusapotiwa na Mama Mwimbaji LUCIE EYENGA alie jiunga na Group AFRICAN FIESTA SUKISA , Mchango huo wala haujasaidia chochote.
Afya ya Dokta NICO KASANDA ikaendelea kuzorota, Serekali ya Rais MOBUTU akitoa Msaada iliapelekwe JIJINI BRUSSELS kwamatibabu zaidi, Ndipo Kifo kikamkuta DOKTA NICO KASANDA akiwa na Umri wa Miaka 49.
DOKTA NICO KASANDA KAWEKA ALAMA KUU KWA ZAMA ZAKE KUHUSU UPIGAJI WA GITA,
KAMWE ATABAKIKUA MMOJA WA NEMBO WA MUZIKI WA CONGO…
Post a Comment