Stori: Ojuku Abraham
WAKATI Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumanne wiki hii alisherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 64, Mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jumatano iliyopita alimpa zawadi baada ya kumvunja mbavu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Katiba Mpya Inayopendekezwa iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete.
Steve, aliyepanda jukwaani kuwakilisha wasanii, alitumia dakika zisizozidi tano kumsifu Rais Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii, akidai ndiye amewafungulia milango ya mafanikio na kwamba watamkumbuka kwa kitendo cha kutambuliwa kwao kikatiba.
Baada ya hapo, mchekeshaji huyo maarufu wa kuiga sauti za watu mbalimbali, alianza kwa kuigiza sauti ya Rais Barack Obama wa Marekani, akimuigiza kumsifu Rais Kikwete kwa kutengeneza katiba mpya na kisha kuwasifu Watanzania na nchi yao kisha akawashukuru kwa kuwaambia asante.
“Mbona hamuitikii jamani Watanzania, au Kiingereza not reachable, naona mna-vibrate tu,” maneno hayo licha ya kuwachekesha mamia ya waliomsikiliza, pia walimfanya Rais Kikwete na Dk. Shein, kuvunjika mbavu hadi kulazimika kulalia meza zao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment