Wafuasi wa Chadema wakijiandaa kuwapokea wanachama wao baada ya kuachiwa huru.…
Wafuasi wa Chadema wakijiandaa kuwapokea wanachama wao baada ya kuachiwa huru.
Halimamdee akisalimiana na wanachama wake baada ya kuachiwa huru
Wakili wakujitegemea wa chadema peter kibatara akizungumza na waandishi wa habari
wafuasi wa chadema wakionyesha bango lenye ujumbe wa kumpongeza mbunge wao
mdee akiwa juu ya gari akitoka nje ya mahakama
gari la wanachama wa chadema likitoka nje ya mahakama
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.
Post a Comment