0

VIDEO YA FERRE GOLA AKIWA NYUMBANI KWAKE


Kwenye Video hii FERRE GOLA kafanya mahojiano na Mtangazaji International LUMBU BAWU akiwa Nyumbani kwake JIJINI KINSHASA,

FERRE GOLA kajibu maswali Mengi yakiwemo :
1. Unalionaje hilo Swala la Mtu kukuchukulia Wanamuziki wako ?  / FERRE GOLA : Unacho takiwa kuelewa ni kwamba Baadhi ya Wanamuziki wingi ambao walichangia kwenye Album ” BOITE NOIRE ” bado wapo kwenye Group. Wale walioondoka Mchango wao kwenye ” BOITE NOIRE ” ulikua Mdogo sana.Kwenye Group langu kwanza ni Mimi, hakuna atakae niyumbisha, Nyimbo nyingi hua nazitayarisha nikiwa Ulaya, nakuja nazo KINSHASA, nawagea ” Vocal “. Sehemu nyingi nachangia mwenyewe. Mimi ndo nawasikitikia hao, naona hawaja tafakari vizuri vipi yatakavyo kua Maisha yao ya Baadae, wala siwatakie Ubaya wowote, Nawaombea Kwa Mungu awafariji Mambo yao yawe mazuri..

2. Tuambie FERRE GOLA ni hasa kilicho wapelekea Vijana hao kuondoka kwenye Group ? nawataja hasa  CHIKITO na NICODEM.  /

FERRE GOLA : Mbona kabla yao wapo wengi walio jiondoa?  akina VIBRATION, SESELE,na wengine wengi, kwa taarifa yako Wapo Wengi wanaoondoka na Wanarudi, Wanajua kwamba hapa ni Nyumbani kwao, Mlango upo Wazi kwa wakati wowote ule . kilichokua cha muhimu nikuona Group inaendelea vizuri, Namimi Mwenye niko vizuri kiafya, Hapa si unaona nimewakaribisha Nyumbani kwangu ? Mnaona wenyewe nilivyo .

3. Tufafanulie kuhusu Kijana RICE MATADIEN ambae kajiondoa kwa WERRASON na kaja kujiunga na Group lako .

FERRE GOLA / RICE nikijana Mzuri kwamuonekano wake, na pia ni Mwimbaji mzuri, Ni Kijana mwenye heshima kabisa. Kama kawaida, Sisi wenjeji wa Mji wa MATADI hua watulivu na hatuna tabia ya Utovu wa nidhamu.

4. Yasemekana kwamba siku hizi FERRE GOLA kawa Mtu wa Malumbano sana, hunatena heshima kwa Kaka zako kwenye Muziki,kwakua umeshakua mwenye mafaanikio.

/ FERRE GOLA : Mbona ninao Uhusiano mzuri na Kakazangu wote? FELIX WAZEKWA tunaelewana vizuri, KOFFI OLOMIDE, tupo sawa kabisa naye, Hata Kaka zangu wa WENGE maelewano yako mazuri.

Kilicho cha Muhimu hapa ni kwamba kila mmoja anajitegemea kivyake,kila Mtu na Mambo yake, Kila mmoja wetu anakabiliana na Maisha kwa namna yake . Huo Mda wa Malumbano sinao tena.

Tusiwachukulie Mashabiki wetu kama Mambumbumbu, hapana , ni Watu na akili zao timamu. kwahiyo Msinitegemee tena kuniona napita kwenye TV na Radio nikiongea Ujinga. Mtu si Maneno bali nivitendo.

Muziki nikuelemisha pia Umma!!! Tunaiwakilisha vilivyo Inchi yetu Inje ya Mipaka na Tunakubalika . Tunazunguuka Dunia nzima, JOHANNESBOURG, COTE D’IVOIRE, Unavyo niona hapa nimerudi safarini nikitokea CUBA.

KAKA ZANGU  KAMWE WATABAKI KUA KAKA ZANGU, KADHALIKA WADOGO ZANGU PIA. SINA TABIA YA MALUMBANO, MIMI NI MCHAPA KAZI, NA MATUNDA KUTOKANA NA KAZI YANGU YANAONEKANA!!!.

Post a Comment

AddThis

 
Top