FC Barcelona jana usiku ilicheza mechi yake ya 7 katika ligi kuu ya Hispania bila kupoteza mchezo wowote, wakishinda mechi 6 na kutoa sare moja.
Lionel Messi alifunga goli lake 402 tangu aanze kucheza soka la ushindani na baadae akamtengenezea Neymar aliyehitimisha ushindi wa 2-0 dhidi ya Rayo Vallecano.
Kutokana na ushindi huo kikosi cha Luis Enrique sasa kimefanikiwa kuwa timu ya kwanza katika historia ya La liga kucheza mechi 7 za mwanzoni mwa ligi hiyo bila kuruhusu wavu wao kugushwa.
Pia wakati huo huo golikipa wa timu hiyo, Mchile Claudio Bravo ameweka rekodi mpya ya katika kulinda lango lake.
Bravo amevunja rekodi ya kucheza dakika nyingi bila kuruhusu wavu wake kuguswa, mpaka kufikia sasa Bravo amecheza jumla ya dakika 561 bila kufungwa goli, akivunja rekodi ya golikipa wa zamani wa Barca, Pedro Artola aliyecheza kwa dakika 560 bila kufungwa goli katika msimu wa 1977-78.
Post a Comment