0
Stori: Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha
BETHIDEI ya msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma imegeuka kuwa maumivu baada ya kumkumbuka aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ukumbini.

Sherehe hiyo ya kuzaliwa ya nyota huyo ilifanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wenzake wa filamu.
Wastara ambaye alionekana kama bibi harusi jinsi alivyopendeza, baada ya burudani ya muziki kupita, watu wote walisimama na kuomba dua kwa ajili ya marehemu wote akiwemo Sajuki, ndipo Wastara alipoingiwa na huzuni kubwa huku machozi yakimlengalenga baada ya kusikia jina hilo la marehemu mumewe.


“Ukweli namshukuru sana Bond kwani kama siyo yeye nisingefika hapa nilipo, amekuwa akinishauri na kunisimamia katika kazi zangu za sanaa,” alisema Wastara.
Baada ya hapo, Bond naye alipewa nafasi ya kuzungumza ambapo naye akammwagia sifa Wastara.
“Wastara ni mwanamke mwenye sifa za kuitwa mwanamke na ninajivunia kufanya naye kazi kwani anajitambua na anaelewa anachoelekezwa,” alisema Bond

Katika sherehe hiyo, msanii Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wake Chuchu Hans walikuwa kama kumbikumbi kwani waliingia wakiwa wameshikana mikono huku wakiitana mume, mke na kuzunguka pamoja wakiwa wameshikana viuno.

Mastaa kibao walihudhuria akiwemo, JB, Flora Mvungi, Sajent, Nisha, Mzee Chilo, Dude, Tito, Kupa, Cathy na wengine wengi huku upande wa burudani, mwimbaji wa Taarab, Amigo akitumbuiza.

KWA UPANDE WAKE JB:WASTARA ANAJITAMBUA 
BONGE la Bwana, Jacob Stephen ‘JB’ amewaasa wasanii wa kike akiwataka wajitambue ili waweze kuishi kwa muda mrefu katika gemu la sanaa.

 Akizungumza katika sherehe ya kuzaliwa msanii Wastara Juma alisema, wasanii wengi wa kike wana muda mchache sana kwenye tasnia ya sanaa, ila kwa Wastara kajitahidi sana na bado anaendelea kuishi katika sanaa kutokana na kujitambua kwake.

 “Nawasihi wasanii wengine wa kike kuiga maisha ya Wastara pamoja na misukosuko ya maisha ya hapa na pale lakini bado anajitambua, anapigana na kusimama, ujue wanawake muda wao ni mchache katika sanaa tofauti na wanaume lakini kwa Wastara bado yuko,Happy birthday Wastara,’ alisema JB.


Post a Comment

AddThis

 
Top