Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, Zacharia Hans Poppe
MASHABIKI na wadau wengi wa soka nchini Tanzania wanapenda sana kuona mpira wa miguu unapiga hatua na kufikia kiwango cha juu kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa ya Afrika hususani Afrika Magharibu.
Ni ukweli kuwa soka halina njia ya mkato kufikia malengo. Lazima kuwepo na mfumo sahihi wa kutunza na kuendeleza vipaji vya soka hasa soka la vijana na mfumo mzuri wa uongozi au utawala.
Nchi nyingi zilizoendelea katika soka duniani kama vile Hispania, Uholanzi, Ujerumani, Brazil na nyinginezo zimeweka watu sahihi katika maeneo sahihi.
Waliandaa mpango mkatati wa kitaifa kwa soka la vijana na kutekelezwa kwa ufanisi na hatimaye wamefika hapo walipo.
Soka la Tanzania kiukweli lina changamoto nyingi kuanzia mfumo mzima wa kutunza vipaji, uongozi wa vyama na klabu kuanzia madaraja ya chini mpaka juu.
Simba na Yanga ni klabu mbili zinazobeba utambulisho wa Tanzania kimataifa. Azam wameanza kuja kwa mbali na kadiri miaka inavyokwenda wanazidi kujitangaza kimataifa kutokana na uwekezaji mkubwa walionao katika soka na mfumo mzuri wa utawala.
Huwezi kuzungumzia Soka la Bongo usitaje Simba na Yanga. Hizi ni klabu zinazochukuliwa kama ‘’Tunu’ ya Taifa.
Lakini kuna changamoto nyingi sana katika klabu hizi ambazo kwa asilimia kubwa zinachangia wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’.
Kuna mitazamo mingi juu ya klabu hizi na kila mtu anakosoa kadiri awezavyo, lakini waliowengi wakati fulani huendeshwa na mitazamo binafsi, masilahi binafsi, chuki na kutumiwa na watu.
Najua yapo mapungufu mengi katika klabu hizi kuanzia utawala na namna wachezaji wanavyopatikana, lakini kuna wakati fulani viongozi wa timu hizi wanalazimika kufanya kazi kwa kutumia mazoea au kulazimishwa na mfumo uliopo katika soka letu.
Atatisha tena?: Mfungaji bora wa ligi kuu soka Tanzania Bara Msimu uliopita, Mrundi, Amiss Tambwe
Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuwashauri viongozi wa Simba na Yanga kuanzisha mfumo na falsafa rasmi ya klabu hizo. Kuna haja ya kujenga misingi bora ya soka la vijana ili kupata muendelezo wa wachezaji.
Klabu kama Barcelona imefanikiwa sana kwa kuwekeza katika soka la vijana, siwezi kuifananisha na Simba au Yanga kwasababu kuna utofauti mkubwa wa uchumi baina ya timu hizi.
Kuna wakati mimi napinga sana kufafanisha soka la Ulaya na Tanzania. Wenzetu wameendelea miaka mingi iliyopita na wamewekeza fedha nyingi katika soka la Tanzania. Lakini kuiga baadhi ya mambo na kwenda nayo ‘Mdogo mdogo’ sina tatizo hapo, ni muhimu sana.
Kutokana na uwezo wao wa kiuchumi wanaweza kuwatunza vijana kwa muda wote, lakini kutokana na hali ya uchumi wa Simba na Yanga, bado kuna tatizo la kuwatunza na kuwaendeleza vijana na kwa bahati mbaya klabu hizo hazina akademi.
Naamini katika klabu ya Simba kuna watu wenye mitazamo mizuri katika soka la vijana kama vile makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
Kaburu ni mtu ninayemkubali sana inapofika hoja ya soka la vijana. Katika uongozi wa Ismail Aden Rage alijitahidi kuboresha soka la vijana akisaidiana na watu kama kocha Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na mjumbe wa kamati ya ufundi kwa wakati huo, Ibrahim Masoud ‘Maestro’.
Mpango ule ulizalisha vijana wengi ambao wanatumika kwa sasa, mfano Haroun Athuman Chanongo, Ramadhan Singano ‘Messi’, Wilium Lucian ‘Gallas’, Said Ndemla na wengineo.
Ataendeleza jitihada za soka la vijana?: Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
Kuna wakati mipango ya akina Kaburu ‘inafeli’ kwasababu ya uwezo mdogo wa klabu kiuchumi. Naamini kuna baadhi ya mambo yanafanyika kwa watu binfasi kutumia fedha zao za mfukoni, na kwasababu mtu anaweza kuwa nacho leo na kesho akakosa, basi mambo yanaharibika.
Kwa bahati mbaya sana watu wengi wanakosoa bila kutoa hoja mbadala. Leo hii mtu anafanya jitihada binafsi kuisaidia Simba au Yanga kwa kutumia fedha zake, watu hawaheshimu, bali wanakazania kukosoa kila kitu.
Kama mtu anakosoa mfumo mbaya uliopo Simba na Yanga na taifa zima huwa namuunga mkono kwa asilimia ‘800’, lakini linapokuja suala la mtu binafsi hususani anayesaidia mambo muhimu kwenda siungi mkono.
Kwa muda mrefu sasa, Simba inawetegemea wafadhili kuendesha mambo yake hususani kundi la Marafiki wa Simba ‘Friends of Simba, F.O.S’.
Kuhusu kundi hili kila mtu anasema lake, wapo wanaosema lina maana kubwa Simba na wengine wanadai linaitumia klabu kujipatia masilahi binafsi.
Hii ni mitazamo tu. Unajua wanapoishi wengi huwa kunakuwa na mitazamo tofauti. Kila mtu anatoa hoja zake na kutetea. Wanaosema F.O.S hawafai wana hoja zao na wanaosema wanafaa wana hoja zao.
Kinachoonekana ni kutofautiana mitazamo, na sio dhambi, lakini siku zote kama watu wanatofautiana kitu fulani, ujue kuna ukweli upo katikati.
Ukweli huwa unabaki kuwa ukweli tu hata kama mtatoana povu kubishana. Lakini binafsi naamini kuwa F.O.S ni kundi muhimu sana kwa klabu ya Simba na lisiangaliwe kwa mtazamo hasi tu bali hata chanya liangaliwe pia.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5475#sthash.8nUKcc8A.dpufAtaendeleza jitihada za soka la vijana?: Makamu wa Rais wa Simba sc, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
Kuna wakati mipango ya akina Kaburu ‘inafeli’ kwasababu ya uwezo mdogo wa klabu kiuchumi. Naamini kuna baadhi ya mambo yanafanyika kwa watu binfasi kutumia fedha zao za mfukoni, na kwasababu mtu anaweza kuwa nacho leo na kesho akakosa, basi mambo yanaharibika.
Kwa bahati mbaya sana watu wengi wanakosoa bila kutoa hoja mbadala. Leo hii mtu anafanya jitihada binafsi kuisaidia Simba au Yanga kwa kutumia fedha zake, watu hawaheshimu, bali wanakazania kukosoa kila kitu.
Kama mtu anakosoa mfumo mbaya uliopo Simba na Yanga na taifa zima huwa namuunga mkono kwa asilimia ‘800’, lakini linapokuja suala la mtu binafsi hususani anayesaidia mambo muhimu kwenda siungi mkono.
Kwa muda mrefu sasa, Simba inawetegemea wafadhili kuendesha mambo yake hususani kundi la Marafiki wa Simba ‘Friends of Simba, F.O.S’.
Kuhusu kundi hili kila mtu anasema lake, wapo wanaosema lina maana kubwa Simba na wengine wanadai linaitumia klabu kujipatia masilahi binafsi.
Hii ni mitazamo tu. Unajua wanapoishi wengi huwa kunakuwa na mitazamo tofauti. Kila mtu anatoa hoja zake na kutetea. Wanaosema F.O.S hawafai wana hoja zao na wanaosema wanafaa wana hoja zao.
Kinachoonekana ni kutofautiana mitazamo, na sio dhambi, lakini siku zote kama watu wanatofautiana kitu fulani, ujue kuna ukweli upo katikati.
Ukweli huwa unabaki kuwa ukweli tu hata kama mtatoana povu kubishana. Lakini binafsi naamini kuwa F.O.S ni kundi muhimu sana kwa klabu ya Simba na lisiangaliwe kwa mtazamo hasi tu bali hata chanya liangaliwe pia.
Yawezekana wanatumia mfumo mbovu kuisaidia Simba, na kama tatizo ni mfumo ndio unawafanya wasiaminike kwa baadhi ya watu, hapo sina tatizo, lakini kusema hawana maana sidhani.
Hebu fikiria watu kama Zacharia Hans Poppe, kwa uwezo alionao kiuchumi, anaweza kukaa nje ya Simba bila tatizo lolote, lakini kutokana na kuipenda klabu hii, anajikuta kila kukicha anaihangaikia.
Ukweli upo wazi, Hans Poppe katoa fedha nyingi sana na anaendelea kutoa ili kuijenga Simba. Yawezekana watu wanaamini ana masilahi binfasi, lakini ukweli unabaki kuwa mtu huyu anatoa hela nyingi hata kuliko anazoweza kuchukua Simba kama watu wanavyodhani.
Leo hii akaunti ya Simba sidhani kama ina fedha nyingi za kusaidia kila kitu, lakini uwepo wa watu kama Hans Poppe unafanya mambo muhimu yaende.
Kwasasa usajili unaendelea katika klabu ya Simba, Hans Poppe ndiye mwenyekiti wa kamati ya usajili. Jitihada zake zinaonekana wazi, amekuwa akihangaika huku na kule kutafuta wachezaji.
Kwa bahati nzuri kila ninapopata nafasi huwa nampigia simu keptein huyu wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania kujua machache kuhusu harakati zake za usajili, hata yeye anaweza kuwa shahidi mzuri kwa hili.
Ni mtu anayesafiri mara kwa mara kutafuta wachezaji. Sidhani kama safari zote analipwa na Simba. Ni mapenzi makubwa aliyonayo katika klabu hiyo, ni mwanachama halisi, anatoa bila kusubiri faida yoyote.
Juzi juzi tu, Hans Poppe alikuwa kushuhudia michuano ya kombe la Kagame inayoendelea mjini Kigali, Rwanda. Nilijua kuwa lengo la mwanajeshi huyu wa zamani lilikuwa ni kupepesa macho ili kuona kama anaweza kupata angalau mchezaji mmoja.
Kwanini anatafuta mchezaji mwingine? Sababu ni rahisi tu, kuna mapungufu yapo ambayo si rahisi kuyajua bila kumuuliza yeye kama mwenyekiti wa kamati ya usajili au benchi la ufundi.
Hans Poppe aliwahi kunieleza kuwa Gilbert Kaze aliyesajiliwa kutoka Vital’O ya Burundi aliomba kuondoka. Kaze kwa muda mrefu alisumbuliwa na majeruhi, hivyo Simba wakamruhusu kuondoka kwasababu asingewasaidia kwa msimu ujao.
Kitasa: Donald Mosoto anasemekana kuondoka Msimbazi
Juzi juzi tu nimesikia kuna mchezaji wa kigeni ambaye ameomba kwenda kucheza soka la kulipwa na taarifa zinaeleza kuwa ni Donald Mosoto, raia wa Kenya. Simba ninavyoifahamu mimi, ni klabu inayofanya vizuri linapokuja suala la kuruhusu wachezaji kutafuta maisha sehemu nyingine.
Wachezaji wengi wameenda kutafuta maisha nje ya nchi kupitia Simba. Mchezaji kama vile Mbwana Samatta, Mwinyi kazimoto wote walitokea Simba na waliruhusiwa vizuri tu.
Ipo idadi kubwa sana, Henry Joseph Shindika, Haruna Moshi, Shaaban Kisiga, Dani Mrwanda na wengine wengi walienda kucheza soka la kulipwa wakitokea Simba.
Simba haina utamaduni wa kuwabania wachezaji, na ndio maana linapotokea suala la Mosoti kuomba kuondoka, hakuna ubishi hata kama ni mchezaji muhimu.
Kwa kuzingatia upungufu unaoenda kujitokeza, Hans Poppe kama mwenyekiti wa kamati ya usajili alishauriana na wenzake (sina uhakika na benchi la ufundi) kuwa aende Kagame kutafuta mbadala wa Mosoti.
Katika mashindano haya yanayoendelea Kigali, Mkurugenzi wa zamani wa ufundi wa TFF, Sunday Kayuni yupo. Hans Poppe alimuona beki mmoja wa klabu ya Telcom ya Djibout, Butoyi Hussein.
Hakuwa na muda wa kupoteza, akajaribu kumuuliza mtaalamu Kayuni ambaye alimhakikishia kuwa ni beki mzuri kwasababu alionekana kucheza vizuri.
Inawezekana timu inayochezea haina kiwango kizuri na haikufika mbali, lakini kuna jambo moja katika mpira linaitwa kipaji binafsi ‘Individual Talent’. Timu inaweza isiwe nzuri, lakini mchezaji mmoja akawa mzuri.
Ndio maana TP Mazembe walimuona Samatta akiwa na timu ya Simba ambayo haikufika mbali. Wakamsajili na anawasaidia mpaka sasa.
Mazembe hawakuangalia kiwango cha Simba kama klabu, lakini waliangalia uwezo wa Samatta waliyemuona katika mechi mbili, Lubumbashi na Dar es salaam.
Kwahiyo kwa suala la Butoyi kuonwa katika mechi mbili si geni. Anaweza kuwa mchezaji mzuri kwa Simba, ingawa sio lazima.
Mbwana Samatta (kushoto) na Patrck Ochan (kulia) waliuzwa TP Mazembe kutokea Simba sc
Baada ya yote, Hans Poppe aliamua kumsafirisha kuja kufanya majaribo. Maana yake anaweza kusajiliwa au hapana, kutegemeana na kocha Patrick Phiri atasemaje.
Kwa hili sioni kama Hans Poppe amekosea kwasababu ndio utaratibu wa timu za Tanzania inapofika kutafuta wachezaji wa kigeni.
Wenzetu wameendelea sana. Ni mara chache kuwajaribu wachezaji wa kuwasajili, lakini kama wanataka wachezaji vijana wa kuwaendeleza katika akademi zao, mara zote wanawachukua maeneo mbalimbali hususani ligi za chini na mashindano ya vijana kisha wanawajaribu na kuwachukua.
Kwa wachezaji wa timu za kwanza, mara zote wanasajili moja kwa moja. Wanaweka dau mezani na kukubaliana na timu inayommiliki na mambo binafsi na mwanandinga huyo, kisha anapimwa afya, akifuzu anasaini mkataba. Haya yanawezekana kwasababu ya maendeleo makubwa waliyonayo pamoja na ligi zao kuoneshwa duniani kote.
Kwetu Afrika usajili wa hivi huwa ni mara chache kufanyika. Huwezi kusema leo hii utaitazama ligi ya Ivory Coast, Mali, Nigeria na kwingineko kiundani ili kuona wachezaji wa kuwasajili moja kwa moja.
Hakujawa na mfumo wa kuwaona vizuri na njia rahisi ni kutafuta wachezaji na kuwafanyia majaribio kama wafanyavyo akina Hans Poppe na kamati yake kwa kushirikiana na benchi la ufundi.
Sioni shida kwa Butoyi kuletwa na Hans Poppe . Mwenye uwezo wa kujua kama anaweza kutumika ni mtaalamu Patrick Phiri.
Atarudi rekodi ya 2009?: Kocha mkuu wa Simba Patrick Phiri ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya wachezaji
Binafsi naheshimu sana jitihada za Hans Poppe katika usajili wa Simba. Anafanya kazi nzur, lakini nashauri kufanyika jitihada ili kutafuta mfumo sahihi wa kusajili wachezaji.
Yawezekana isiwe leo wala kesho, lakini mfumo wa kuwaleta wachezaji wengi wa kigeni, kuwapangia hoteli, kuwalisha chakula, kuwasafirisha na kuwapa posho wakati wa majaribio sio jambo la kuendelezwa sana.
Siku za usoni nitatamani Simba ipige hatua na kuweka watu maalumu wa kuzungukia maeneo tofauti barani Afrika kutafuta wachezaji na sio kuwaleta kwa ajili ya majaribio.
Siwezi kumpinga Hans Poppe kwasababu mfumo ndio unamfanya afanye hivyo na asipofanya hivyo, maana yake Simba haitapa wachezaji wa kigeni.
Kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni kulundikana Simba au Yanga sio sababu ya kudidimiza soka letu. Hata tusema wachezaji wa kigeni wasiwepo, soka la Tanzania litabaki kuwa nyuma.
Tatizo la msingi sio idadi ya wachezaji wa kigeni, tatizo lipo kwenye mfumo wetu. Mbona kuna timu za ligi kuu hazina wachezaji wa kigeni, lakini haziendelei.
Kama taifa, tunatakiwa kurudi nyuma na kuwa na mpango mkakati wa kitaifa wa kujenga mfumo imara wa soka la vijana na tukifanya hivyo na kushindwa kupata mafanikio, basi turudi kujadili wachezaji wa kigeni.
Naamini kama tutarudi kwenye soka la vijana tutaendelea.
Sina tatizo na Hans Poppe na namna anavyopata wachezaji, lakini nina tatizo na mfumo mzima wa soka la Tanzania.
Sijui kama kweli kamati hizi za usajili kwa asilimia mia moja zinasajili kwa matakwa ya mabenchi ya ufundi. Kuna wakati malalamiko yanasikika kutoka kwa makocha, lakini haya yanatokea kutokana na mfumo wetu mbovu.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba mpaka sasa ni Mganda Joseph Owino, Wakenya, Donald Mosoti na Paul Kiongera. Pia wapo Warundi wawili, Amiss Tambwe na Pierre Kwizera.
Tayari Simba imekamilisha idadi ya wachezaji wa kigeni, lakini mwenyekiyi wa Kamati ya usajili Zacharia Hans Poppe amesema kuna mchezaji mmoja ameomba kuondoka, hivyo kama Butoyi atafuzu majaribio atapewa mkataba.
Post a Comment