0
Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii. Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji wanaondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili.
Shinji anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £8m.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund.
Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m.

Post a Comment

AddThis

 
Top