0
                      Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.              


KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani pamoja na dereva wake Nuaka Seme wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.
Akiongea na vyombo vya habari huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hana ruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George Stephano Matiko (24)
.




"Ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.
Aliongeza kuwa;
" Mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".

Kwa upande wake Afisa muuguzi wa hospitari hiyo Bw. Denis Haule alisema kuwa majeruhi wawili walipokelewa majira ya saa tano usiku na mwingine alikuwa amekwisha fariki dunia na kubainisha kuwa hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri na Kamanda wa Polisi anaweza kuruhusiwa muda wowote.
"tumewapokea jana usiku majeruhi wawili na mmoja akiwa amekwisha fariki dunia , hali yao kwa sasa inaendelea vizuri na kamanda anaweza kuruhusiwa wakati wowote....lakini dereva wake anatakiwa kuendelea kupewa matibabu kutokana na maumivu mbalimbali katika mwili wake

Post a Comment

AddThis

 
Top