0
Matokeo mabaya: Manchester United walipoteza kwa mabao 2-1 mechi ya ufunguzi, ligi kuu nchini England dhidi ya Swansea katika uwanja wa Old Trafford.

MANCHESTER United ipo hatarini kuingia katika mgogoro tena baada ya mashabiki waliokosa uvumilivu kupanga kufanya maandamamo makubwa wakipinga kitendo cha wamiliki wa klabu hiyo, Familia ya Glazer kushindwa kuwekeza katika kikosi.
Mashabiki hao wanashinikiza wamiliki kuondoka Old Trafford kama watashindwa kusajili nyota wapya.
Zikisalia siku 10 dirisha la kiangazi la usajili kufungwa, Lous Van Gaal bado ana kikosi dhaifu na anahitaji kusajili ili kuingia katika ushindani wa ligi kuu.
Makama mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward bado ana matumaini ya kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo, wakati huo huo akiamnini kuwa wataweza kumshawishi Angel di Maria kutua Old Trafford kutokea klabu yake ya sasa ya Real Madrid.
Pia wanamhitaji beki wa Ajax ya Uholanzi, Daley Blind
Mashabiki hawana furaha: Sehemu ya mashabiki wa Man United wanaoweza kuandamana dhidi ya familia ya  Glazer kwenye mechi na QPR  
Mashabiki wa Manchester United hawana furaha na wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glaze 

Hali ngumu: Louis van Gaal anajua kuwa anahitaji kuongeza wachezaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa

Post a Comment

AddThis

 
Top