0
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Makaburi ya Makamba Msakuzi, Mbezi jijini Dar es Salaam ambapo wananchi hao waligundua kuwa  maiti ya kijana huyo iliweka ndani ya jeneza kinyume na utaratibu uliozoeleka yaani kichwa chake kilielekezwa sehemu ya miguu na miguu ilielekezwa sehemu ya kichwa.

Msafara wa kuelekea makaburini kwa ajili ya mazishi ya Michael Krisanto.
\Kama hiyo haitoshi, maiti hiyo badala ya kuviringishwa sanda nyeupe, ilitumika sanda nyeusi kitu  kilicholeta tafsiri tofauti miongoni mwa waombolezaji.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, kabla jeneza lenye mwili kutumbukizwa kwenye kaburi kulitokea mvutano mkubwa baina ya wanandugu na waombolezaji.
Waombolezaji wakizozana juu ya utaratibu wa mazishi ya Michael Krisanto.
Imeelezwa kuwa, waombolezaji hao waliwataka wanandugu wafuate taratibu zilizozoeleka katika jamii wakati wa kuzika.Hata hivyo, ndugu wa marehemu hawakuwasikiliza na kudai kwamba walikuwa wanafuata mila na tamaduni za kabila lao (jina la kabila linahifadhiwa kwa sababu maalum).

Mwili wa marehemu, Michael Krisanto ukishushwa kaburini.
Wanandugu hao wakaamua kushusha jeneza lenye mwili kaburini na walipoanza kuzika waombelezaji walikuja juu na kulitoa jeneza kaburini hali iliyosababisha kutokea kwa vurugu kubwa.


“Vurugu hizo zilisababisha wanawake waliokuwa makaburini kutimua mbio na wanaume wakasusa na kuwaacha wanandugu waendelee kumzika ndugu yao,” alisema shuhuda  wa tukio hilo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.

Post a Comment

AddThis

 
Top