Bondia Stevin Kobelo kushoto akirusha ngumi kumpiga Karim Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara park manzese Dar es salaam, mpambano huo walitoka droo ya kufungana point
Mabondia Joseph Gili kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa manyara park manzese Dar es salaam , Tamba alishinda kwa T.K.O ya raundi ya nne
Bondia Julius Kisalawe kushoto akipambana na Ramadhani Kumbele wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam, Kumbele alishinda kwa pointi na kufanikiwa kuchukua ubingwa
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli ‘Masta’ kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia Ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point kushoto ni Refarii Ally Bakari
Post a Comment