0


Wakati viongozi mbalimbali Duniani walipokuwa kwenye maadhimisho ya kufurahia maisha ya kiongozi wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela,
mitandao ya kijamii nayo ilikuwa na yake zaidi ya kufatilia na hasa juu ya watu binafsi na maisha yao yanavyokwenda.

Rais wa Marekani, Barack Obama, alifanikiwa kupanda kwenye jukwaa la uwanja wa FNB na kumuelezea Mandela kwa namna ya kipekee kwenye hotuba aliyoitoa, ila si mara moja ni zaidi ya mara mbili kuna matukio yaliyochukuliwa kwa picha ambayo kidogo yalileta hisia tofauti kwa wadaku mbalimbali.

Kwanza kulikuwa na picha ya Obama akionekana kusalimiana kwa kushikana mkono na Rais wa Cuba Raul Castro. Kisha kulikuwa na ile ambayo ilipigwa ikimuonyesha Obama akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Bi. Helle Thorning-Schmidt picha mabayo walionekana wakiwa kwenye tabasamu sambamba na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron.




Baadhi ya mitandao ya kijamii imesema kwamba hakikuwa ni kitu sahihi kupiga picha za namna ile kwenye Ibada ya kumbukumbu hiyo, kwenye picha hizo watu wengi wameonekana kumuangalia zaidi First Lady wa Marekani Michelle Obama, ambaye alikuwa amekaa pembeni ya Obama, huku akionekana kuwa na muonekano wa hasira kwenye uso wake.

Wakati Michelle akionekana kuangalia katikati ya kiwanja, vichwa vya habari na tweets mbalimbali zilikuwa vikimfatilia yeye zaidi kwa muonekano wake wa kutokuwa na furaha tofauti na viongozi wengine waliokuwa wanacheka pembeni yake.

Picha nyingine baadae iliwaonyesha Obama wakiwa wamebadilishana siti, Michelle alionekana akiwa amekaa na Waziri Mkuu huyo wa Denmark na Obama akionekana kuangalia mbele huku sura yake ikionekana kuwa ameboreka. 

Baadae Obama aliposimama wakiwa wanataka kuondoka, Michelle Obama alionekana anaongea na Thorning-Schmidt.



Post a Comment

AddThis

 
Top