0


Baaada ya kuifunga waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano ya Mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Cecafa, timu ya taifa ya Uganda, ' KIlimanjaro Stars', timu ya Taifa ya Tanzania Bara, siku ya kesho watakuwa uwanjani kuwakabili webnyeji wa michuano hiyo ya sasa, ' Harambee Stars' , timu ya taifa ya Kenya katika pambano la kwanza la hatua ya nusu fainali katika uwanja wa Machakos.

     STARS IPO TAYARI
Kuiondosha Uganda katika mchezo wa robo fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penati, kulikuja baada ya wachezaji kucheza soka la kujituma na kufuata maelekezo.

Japo ya makosa ambayo kimsingi hutokea mchezoni hilo ni jukumu la mwalimu kuliweka sawa.

Safu ya ulinzi imeoneka kucheza kwa uangalifu mkubwa, wakati wa mchezo wa kwanza dhidi ya Zambia, uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, kisha ikaonekana kuwa imara zaidi katika mchezo dhidi ya Somalia na baadae Burundi katika hatua ya makundi. Wakati  safu ya mashambulizi ikipoteza nafasi nyingi za kufunga, Stars ilifunga mabao matatu tu katika michezo ya hatua ya makundi, huku ile ya ulinzi ikifanya kazi kubwa.

Kipa, Ivo Mapunda alifanya kazi kubwa katika mchezo wa robo fainali pale alipocheza vizuri kwa dakika zote 90 na baadae kudaka mikwaju miwili ya penati, aliruhusu mabao mawili katika mchezo huo ambao pia safu ya mashambulizi ilifunga mara mbili.
  
Upangaji wake wa safu ya ulinzi umeweza kumfanya awe makini zaidi na ndiyo maana aliweza kuwazima Uganda.

Kiujumla safu yote ya ulinzi imeonekana kucheza kwa umakini mkubwa, ila ni muhimu wakaongeza kila walichokionesha kwa asilimia mia moja ili kuendana na kasi ya Kenya ambayo imekuwa ikiwavuruga wengi na kujikuta wakitoa mikwaju ya penati. Kenya ' butu' katika ufungaji, ila tahadhari tu ni kwamba wanaweza kuwa hatari zaidi mbele yetu. Stars inatakiwa kupandisha kiwango chetu cha umakini, kujituma, na kucheza kwa umoja. Ni wakati wa kulipa kisasi cha mwaka 2002 walipoishinda Stars, mabao 3-2 katika fainali, CCM Kirumba.

SASA NI ZAMU YA THOMAS ULIMWENGU

Ikiwa na mchezaji ambaye tunaweza kusema ndiye kinara wa ufungaji wa michuano hiyo kama kungekuwa na rekodi za kutosha, Mrisho Ngassa, Stars inaye pia Mbwana Samatta, wote hawa tari wamefunga mabao.

Ngassa alifunga bao lake la kwanza kisha akafunga lingine katika mchezo wa robo fainali. Samatta yeye alifunga katika mchezo muhimu dhidi ya Burundi, tukiwa na wafungaji wanne tofauti katika michezo minne iliyopita, ( Said Mourad, aliyefunga dhidi ya Zambia, na Harouna Chanongo, aliyefunga dhidi ya Somalia), sasa ni wakati ambao mfungaji wa tano atatokea. Kama, To atakuwa ' fit' na kucheza itakuwa ni nafasi yake.

ILa endapo litatokea jambo tofauti inaweza kuwa ni nafasi ya Amri Kiemba kufunga bao lake la kwanza.

 Tukiwa na Mbwana Samatta, timu pinzani zote zimekuwa zikimtolea macho hivyo ni jukumu la wachezaji wengine kutumia ' mwanya' huo kufanya mambo makubwa. Kenya wanaye kipa mahiri, Duncan Ochieng, na Stars inaye Ivo Mapunda, makipa wote hawa udakia timu ya Gor Mahia ya Kenya, hivyo endapo Stars itaishia kupoteza nafasi nyingine za wazi ni sawa na kujichimbia ' kaburi' katika mikwaju ya penati.

Ni kujitahidi kuimaliza mechi ndani ya muda wa kawaida na endapo hali itashindikana ni kujitahidi kuongeza umakini katika ' mchezo wa mchezaji, mmoja, mmoja', mikwaju ya penati. \

Kufika fainali itakuwa ni mafanikio ya kusifika kwa Stars, ila matokeo yoyote ya kuondolewa ni mabaya. NI lazima ushindi uje kwa kuwa Stars inakikosi chenye uzoefu zaidi kuliko vyote mwaka huu.

 4-3-3 NDIYO MFUNMO SAHIHI

Stars inao wachezaji wanaokidhi mahitaji ya mfumo huu, kutokewepo kwa kiungo SAlum Abubakary hiyo inamaanisha kuwa kiungo Athuman Idd ' Chuji' ataanza katika nafasi hiyo sambamba na Frank Domayo, na Amri Kiemba, katika safu ya mashambulizi, Samatta, ULimwengu na Ngassa hawa ni wachezaji sita ambaoi wanaweza kuuchezesha mfumo huo kwa usahihi. Nafiki sasa ni wakati wa ' kilimanjaro stars kutwaa taji wakiwa ugenini'.

Post a Comment

AddThis

 
Top