Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Bwana Anselm Lyatonga Mrema amefariki Dunia.
Habari kutoka Dodoma zinasema kuwa Mrema amefariki usiku wa tarehe 10 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amepelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na shinikizo la damu
Aidha kufuatia msiba huo mkubwa uliolikuba Bunge Rais Jakaya Kikwete amemtumia Spika wa Bunge, Anne Makinda salamu za rambirambi akionesha kusikitishwa sana na msiba huo.
Katika salamu zake kwa Spika, Rais Kikwete amemwelezea marehemu kuwa alikuwa ni mtumishi Mwaminifu, Mwadilifu na mchapakazi hodari aliyejituma kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yake.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mtumishi wa Ofisi yako ya Bunge, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Bwana Anselm Lyatonga Mrema kilichotokea usiku wa tarehe 10 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amepelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na shinikizo la damu”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
“Nilimfahamu Marehemu Anselm Lyatonga Mrema, enzi za uhai wake, kama Mtumishi Mwaminifu, Mwadilifu na Mchapakazi Hodari aliyejituma kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yake, sifa ambazo zilimfanya apande cheo kutoka kuwa Katibu Msaidizi Mwandamizi wa Bunge na kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za Bunge”, alisema Rais Kikwete.
Anselm Lyatonga Mrema ni mdogo wa Mbunge wa Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Post a Comment